Mwenyekiti
wa Serikali za Mtaa, Bw. Hassan Chambuso akimuongoza Mhe. Meya wa Manispaa ya Ilala, Jery Silaa kwenda kujionea eneo la kipande cha
barabara ya St. Marys Tabata ambacho kinaleta shida baina ya Mkandarasi
na Dawasa.
Mkandarasi
wa Barabara ya Tabata-St. Mary Bw. George Lupia (wa pili kushoto), akitoa ufafanuzi kwa Meya wa Ilala, Mh Jerry Silaa kuhusu kukwama
kwake kuendelea na ujenzi kutokana na Mabomba ya Dawasa kupita katikati
ya barabara hiyo.
Meya
wa Ilala, Mh. Jerry Silaa akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa
Tabata Bw. Chambuso kuhusu yeye kulifuatilia swala hilo, kwenye Mamlaka
husika haraka iwezekanavyo. Kulia ni Diwani wa Kata ya Tabata St.
Mary's, Bi. Mtumwa Mohamed.
Mkandarasi
Geoge Lupia Akimwelezea Meya wa Ilala Mh Jery Silaa kwamba wametumia
pesa nyingi katika kuchimba eneo hilo na kupata usawa wa Barabara lakini
kikwazo kimekuja baada ya kukuta mabomba ya Dawasa ambayo yamekatiza
katikati ya barabara na pembeni, hivyo kuleta ugumu katika kufanikisha
Umaliziaji wake.
Mkandarasi
wa Manispaaa ya Ilala Bwana Kassim Muhinda Akimwelezea Meya Jerry Silaa
kwamba washaongea na Dawasa lakini hawapewi ushirikiano wa kutosha na
wa haraka katika kushughulikia utoaji wa Mabomba hayo
Mkandarasi wa Manispaaa ya Ilala Bwana Kassim Muhinda akiendelea kufafanua jambo kwa Mh Meya wa Ilala Jerry Silaa
Meya wa Ilala Mh Jerry Silaa Akiongea na vyombo vya habari kutoa ufafanuzi wa nini kitafanyika ili kutatua mgogoro huo.
Diwani
wa Kata ya Tabata -St Mary Bi Mtumwa Mohammed Akielezea ni jinsi gani
wanainchi wa eneo hilo wanapata tabu baada ya barabara hiyo kuchimbwa
hivyo kufanya upitaji wa magari kusitishwa kwa mda eneo hilo
Mkandarasi
wa barabara ya Tabata_St Marys Bwana George Lupia akiongea na vyombo
vya habari kuelezea ni ugumu gani anakumbana nao katika utekelezaji wa
ujenzi wa barabara hiyo,kutokana na mabomba ya Dawasco kupita katikati
ya barabara Hiyo
Hiki
ndio kipande cha barabara ya Tabata-St Marys ambacho
kinashindwa kuendelea na matengenezo kutokana na Mabomba ya Dawasa
kupita kati kati ya barabara na pembezoni,hivyo kumpa hali ngumu
mkandarasi kuchimba eneo hilo ili ajaze kifusi.
Pembenini
maji yaliyotuama baada ya Bomba la Dawasa kupasuka Hivyo kuleta
usumbufu kwa mkandarasi kukamilisha ujenzi wa eneo hilo.
Hilo shimo hapo ni bomba amabalo limepita katikati ya barabara
Mmiliki
wa gari hii ndogo Toyota Premio alipatwa na hasira baada ya Gari yake
kushindwa kupanda ili atokee upande wa pili ikambidi kushuka
Kwa hasira mmiliki huyu akatoa vizuizi ya Barabara hiyo na kuvitupa pembeni
Hapo mmiliki huyo akikagua gari yake kama imepata mikwaruzo
Wakiendelea kutazama gari yao kwa umakini
Akaamua kupanda kwa kasi baaada ya vizuizi kutolewa na yeye mwenyewe.
Meya wa Manispaaa ya Ilala Mh Jerry Silaa ametembelea eneo la Tabata-St Marys kujionea maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo na pia kuweza kuona mabomba ambayo yanaleta mgogoro baina ya mkandarasi na Manispaaa na Dawasa,Akiwa eneo hilo la St Marys Mh Jerry Silaa ameweza kujionea namna mabomba ya Dawasa ambavyo yamepita katikati ya barabara na pembezoni yakiwa katika kima kifupi hivyo kumzuia mkandarasi kuendelea na ujenzi wake.
Akiongea na vyombo vya habari Mh Meya Amesema kuwa barabara hiyo imetumia gharama za takribani bilioni 1 lakini imeshindwa kumalizika kwa wakati kwa sababu ndogo ya Dawasa kutokushirikiana nao ili kuweza kumpa mkandarasi ramani kamili ya bara bara hiyo,Meya Silaa akaongeza kuwa wameshawasiliana na wenzao wa Dawasa kuhusu tatizo hilo lakina wamekuwa hawapewi majibu kwa wakati na ya kuridhisha.
Naye
mkandarasi wa eneo hilo Bwana George Lupia amesema kuwa alipewa ramani
na manispaa ambayo haikuonysha kama kuna mabomba ambayo yamepita
hapo,lakini wakati ameanza kuchimba barabara hiyo ndio akakutana na
mabomba hayo,Mkandarasi huyo akaongezea kwamba alishawasiliana na Dawasa
kitambo sana lakini hapewi majibu ya kuridhisha kuhusu kushirikiana nao
kuhamisha bomba hizo.
Naye Diwani wa kata Hiyo Bibi Mtumwa Mohhamed amesema wanainchi wa eneo hilo wanapata tabu sana kwa kuwa magari yao hayawezi kutoka ndani wala kuingia kwa kuwa barabara imechimbwa kwa kina kirefu sana,hivyo amewaahidi wanainchi wa eneo Hilo kwamba wanaendelea kulitatua tatizo hilo na wenzao wa dawasco ili kuweza kuhamisha mabomba ya eneo hilo. (Picha zote na habari na DJ SEK BLOG)
No comments:
Post a Comment