Mwanajeshi wa Ukraine
Rais wa Ukraine Petro Poroshenko
ameongeza makubaliano ya kusitisha vita na wapiganaji wanaotaka
kujitenga mashariki mwa Ukraine kwa siku tatu nyingine.
Mkataba huo ulitarajiwa kukamilika hapo jana
lakini rais Poroshenko akauongeza baada ya waasi hao wanaozungumza na
wawakilishi wa usalama kutoka ulaya kusema kuwa wako tayari kuongezwa
kwa mda huo.Bwana Poroshenko ameweka masharti katika mda wa masaa 72 yajayo ambayo anatarajia yataafikiwa huku waasi hao wakisema kwamba watatoa mda zaidi kwa mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja.
Wakati huohuo Urusi imetangaza mipango ya kutuma tani 60 za msaada wa kibinaadamu katika eneo la mashariki mwa Ukraine siku ya jumamosi.
Kitengo cha umoja wa mataifa cha wakimbizi kinasema kuwa makumi ya maelfu ya raia wamewachwa bila makao kufuatia mzozo huo swala ambalo rais wa Urusi Vladmir Putin amelitaja kuwa janga la kibinaadamu.
Wito wa Urusi kuitaka Ukraine kuruhusu kuingia kwa msaada huo ni kinyume na onyo lililotolewa na taifa hilo kwamba Ukraine itakiona cha mtema kuni iwapo ushirikiano wa Ukraine na muungano wa ulaya utaathiri uchumi wa Urusi.
No comments:
Post a Comment