TANGAZO


Saturday, June 14, 2014

Mbunge Filikunjombe aandaa semina kwa Viongozi wa CCM Wilaya ya Ludewa

1a  
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai akifungua semina ya wenyeviti, Makatibu na Makatibu Wenezi wa CCM wilaya ya Ludewa inayohusu masuala ya kuimarisha Chama na Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi CCM katika jimbo la Ludewa ambalo linaongozwa na Mbunge wake Machachari na makini Mrh. Deo Filikumbjombe, Semina hiyo imeandaliwa na Mbunge wa jimbo hilo ambayo ilianza na ziara ya kimafunzo ya viongozi hao wa CCM wilaya ya Ludewa ambapo walianzia mjini Dodoma wakitembelea Bunge na Chuo Kikuu cha UDOM na kisha Dar es salaam ambako wanahitimisha na Semina hiyo yenye manufaa makubwa kwa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ludewa. (Picha zote kwa hisani ya Fullshangwe-Dar es Salaam)2a 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai akifungua semina ya wenyeviti, Makatibu na Makatibu Wenezi wa CCM wilaya ya Ludewa 3aMwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ludewa Ndugu Stanley Kolimba akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai ili kufungua rasmi semina hiyo ya kimafunzo kwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ludewa. 6a 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai akisalimiana na Matson Chizii Mkurugenzi wa Uchaguzi Mstaafu CCM ambaye alikuwa mkufunzi wa mafunzo hayo. 7a 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai kulia akiongozana na Mbunge wa jimbo la Ludewa na muandaaji wa semina hiyo ya kimfunzo kwa viongozi wa CCM wilaya ya Ludewa Mh. Deo Filikunjombe. 8a 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai kulia akiongozana na Mbunge wa jimbo la Ludewa na muandaaji wa semina hiyo ya kimfunzo kwa viongozi wa CCM wilaya ya Ludewa Mh. Deo Filikunjombe. 10a 
Matson Chizii Mkurugenzi wa Uchaguzi Mstaafu CCM kulia akinyanya mkono juu wakati washiriki wa semina hiyo wakiimba wimbo maalum wa CCM 16a 
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiimba wimbo 18a 
Baadhi ya washiriki wakiwa katika semina hiyo .

No comments:

Post a Comment