Awamu mpya ya mazungumzo
yanayolenga kumaliza mapigano ya miezi sita nchini Sudan Kusini
imeahirishwa mara moja baada ya serikali na waasi kutoa masharti mapya.
Hatua hiyo inajiri wiki moja tu baada ya Rais
Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar kukubaliana kubuni serikali
ya mpito katika kipindi cha miezi miwili ijayo.MKuu wa ujumbe huo Michael Makuei amesema kuwa wanangojea msamaha kutoka kwa bodi inayosimamia mazungumzo hayo,IGAD na Balozi Mahboub Maalim aliyemwita Rais Salva Kiir Mjinga.
Kwa upande mwengine waasi nao wanataka pande zaidi kuhusishwa katika mazungumzo hayo wakiwemo wafungwa wa zamani pamoja na viongozi wa dini.
Viongozi wa eneo hili wametishia kuziwekea vikwazo pande pinzani katika mazungumzo hayo iwapo zitashindwa kuafikiana kisiasa.
Maelfu ya watu wamefariki huku zaidi ya watu milioni moja wakitoroka makaazi yao tangu vita hivyo vianze mnamo mwezi Disemba.
Kwa sasa mashirika ya misaada yameonya kuzuka kwa baa la njaa.
No comments:
Post a Comment