WAZIRI mkuu wa zamani Edward Lowassa na wabunge
mbali mbali wamempongeza mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kwa
jitihada mbali mbali za kuwakomboa wana Ludewa.
Lowassa ambae ni mbunge wa jimbo la Monduli alitoa pongezi
hizo mjini Dodoma juzi nje ya ukumbi wa bunge wakati akisalimiana na viongozi
wa CCm ngazi ya kata zaidi ya 92 waliofika bungeni kushuhudia shughuli za bunge
kwa mwaliko wa mbunge Filikunjombe.
" Wana Ludewa mna kila sababu ya kujivunia kwa kuwa na
mbunge mchapa kazi ninyi mnamwita Jembe ila mimi namwona zaidi ya jembe ni
katapila na hamkokosea kumchagua nawaombeni mtunzeni mbunge wenu na epukeni na
michepuko kwani ni mbunge makini na anayependa kuwatumikia"alisema Lowassa
Mbunge wa jimbo la mbinga Magharibi kepten John
Komba amempongeza
mbunge wa
jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kutokana na jitihada
mbali mbali anazoendelea kuzifanya
katika kuwatumikia wana Ludewa.
Komba ametoa pongezi hizo juzi
wakati wa hafla fupi ya kuwakaribisha
wajumbe 92 kutoka jimbo la Ludewa
ambao ni wenyeviti kata na makatibu
kata kutoka kata
zote 25 za
jimbo la Ludewa na viongozi wa wilaya
ambao wapo katika
ziara ya
siku nne mjini Dodoma na Dar es Salaam
.
Alisema kuwa jembo
kama Filikunjombe katika historia ya jimbo la Ludewa ni aliyepata kuwa mbunge wa
jimbo hilo marehemu Holace Kolimba na baada ya hapo mbunge mchapakazi ni
Filikunjombe .
“Nasema mmlea Deo Filikunjombe
ni mbunge atakayefanya makubwa jimbo la
Ludewa kutokanana jitihada zako za
kimaendeleo na kazi kubwa anayoifanya ya kuwatumikia
wananchi wa
jimbo la Ludewa ….nataka
kuwaambieni leo viongozi ambao mpo hapa Filikunjombe kwangu mimi
amekuwa msaada mkubwa sana”
Hata hivyo alisema kuwa
jitihada kubwa zimekuwa zikifanywa na Filikunjombe pamoja na wabunge wengine wa
mkoa wa Ruvuma ambao wanazunguka
ziwa nyasa kutokana na adha kubwa ya
usafiri ila kwa sasa kero ya
usafiri ikiwemo ile ya mlima kandamija
Pia amewaonya wana
Ludewa kuacha
kutafuta mbunge kama ndugu yao na badala
yake kumtafuta mbunge wa ajili ya kuwapelekea maendeleo kama ilivyo kwa mbunge huyo ambaye amekuwa ni mwabikaji mzuri kwa
wananchi.
“Mkimuacha Deo
Filikunjombe Ludewa mmekosa mambo na mmekosa maendeleo katika jimbo hilo hivyo ni
lazima kuendelea
kumtunza ili
azidi kuwatumikia zaidi”
Komba alisema kuwa
wilaya ya Ludewa mbali ya kuwa na utajiri mkubwa madini ila wabunge wote
waliopita walikuwa wakizungumzia suala
hilo bila kuonyesha jitihada ila toka
ameingia Filikunjombe madini hayo
yameanza kushughulikiwa .
Alisema kuwa kwa
sasa wananchi
wa Mwambao kilio chao kikubwa ni
meli na kuwa
tayari wabunge wote wa Mwambao
wameungana kuona wanapigania upatikanaji
wa meli
hiyo ili kutatua kero ya usafiri ziwa Nyasa .
“Mwisho nasema
endeleeni kumpatia ubunge Deo Filikunjombe
msibadilishe wabunge kama gauni…wenzetu wa kaskazini
wanatushinda katika hilo mfano Msuya
aliacha ubunge
baada ya kusema mwenyewe sasa basi baada
ya kufikisha maendeleo makubwa ikiwa ni pamoja
na kufikisha umeme hadi chooni ….ila sisi baada ya kipindi kimoja tunasema
aliyevivyo(amekula hivyo hivyo)”alionya Komba
.
Huku kwa upande wake , Mbunge wa Mbinga
Mashariki Gaudence Cassian Kayombo alisema kuwa mbali ya
wana Ludewa kumuona mbunge wao ni jembe ila kwake na
wabunge wengine na kusini wamekuwa
wakimuona ni mkombozi wa maendeleo mikoa
ya kusini.
Kayombo pia
amewaonya wana Ludewa kuachana na tabia ya
kubadili wabunge kama nguo na kuwa iwapo mbunge wao asingekuwa mchapakazi
ni wazi harufu ya upinzani
ingeanza kujitokeza katika jimbo hilo
ambalo limeendelea
kuwa ni tishio hata kwa vyama vya upinzani .
Kwani alisema jitihada
za wana Ludewa
kujaribu kwa
sasa zimefika kikomo baada ya kumpata
mbunge huyo ambae ni mchapakazi mzuri na kuwa ni vema wana
Ludewa hawana haja ya kuendekeza uchoyo .
“Kitu ambacho kitaendelea
kuiweka CCM madarakani ni umoja na mshikamano na bila umoja na
mshikamano hakuna chama na hakuna mbunge ndani
ya CCM”
Kwa upande wake mbunge wa viti maalum mkoa
wa Mbeya Hilda Ngowi mbali ya kumpongeza
mbunge Filikunjombe kwa maendeleo bado
alisema kuwa mbunge huyo ameleta ngunzo kubwa bungeni kwa
kuvunja rekodi ya kukaribisha
wageni wengi
zaidi bungeni tukio ambalo ni la kwanza
kwa mbunge kuleta wabunge wengi kiasi hicho bungeni.
Huku mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati
(CCM) akisema kuwa anatamani sana kufika Ludewa ili kumuunga mkono mbunge
Filikunjombe ambae amekuwa ni ngunzo katika bunge kwa utendaji kazi na kutetea
maslahi ya wananchi wake na Taifa.
Mbunge wa jimbo la Mwibara Kangi
Lugola alisema kuwa kamwe katika ubunge wake hatakuja kumsahau mbunge
Filikunjombe na kudai kuwa lazima viongozi wa kata na wanachi wa jimbo la
Ludewa kuachana na michepuko kwa kutazama huku na kule badala yake kutulia
njia kuu kwa maana ya kuendelea kufanya kazi na Filikunjombe.
Wakati Filikunjombe
akidai kuwa
wito ambao wajumbe hao wameonyesha ni
wito mzuri zaidi na kuwa hilo ni
deni kwake
na malipo yake ni kuwafikishia maendeleo jimboni.
Kwani alisema kuwa kamwe
hatawaangusha katika utendaji kazi wake na kuwa ni lazima aendelee
kufanya kazi kwa moyo zaidi ili kuwapa
imani wananchi.
|
No comments:
Post a Comment