Kundi moja la wanawake walio na
hisia za kimapenzi na mapadre wa kikatoliki wamemuandikia barua kiongozi
wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ya kumtaka kubadilisha sheria
za kanisa hilo zinazowazuia viongozi hao wa dini kuoa.
Wanawake hao 26 kutoka Italy na maeneo mengine
wanasema kwamba wamekuwa wakishiriki ama wanataka kushiriki katika
uhusiano wa kimapenzi na mapadre na kwamba wametoa ombi hilo kwa niaba
ya wanawake wengine ambao wako katika hali kama hiyo.Barua hiyo inazungumzia kuhusu uchungu wa kushindwa kuishi maisha yao kikamilifu mbali na kutaka kukutana na papa Francis.
Papa Francis amekuwa akiunga mkono utamaduni wa useja,lakini mwaka 2010 aliandika akisema kuwa huenda msimamo wake ukabadilika.
Papa francis amekuwa akimtembelea mjane wa aliyekuwa kasisi Jeronimo Podesta ambaye alijiuzulu katika utumishi wake na kuoa, zaidi ya miaka 40 iliopita.
No comments:
Post a Comment