TANGAZO


Wednesday, May 7, 2014

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Shein Azungumza na Uongozi wa Idara Maalum za SMZ Ikulu

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dkt.Ali Mohamed Shein(katikati) akizungumza na Uongozi wa Idara Maalum za SMZ katika mkutano wa utekelezaji mpango kazi wa robo tatu ya mwaka  Julai-Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Unguja leo asubuhi.
Baadhi ya makamanda wa Idara maalum za SMZ wakimsikiliza  Waziri wa Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ,Mhe,Haji Omar Kheri (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji mpango kazi wa robo tatu ya mwaka  Julai-Machi 2013/2014,mbele ya  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dkt.Ali Mohamed Shein,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Unguja leo asubuhi. (Picha na Ramadhan Othman,Ikulu)
                              
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuongeza kasi ya utekelezaji wa majukumu yao ili huduma kwa wananchi ziweze kupatikana kwa mujibu wa malengo yaliyowekwa.
Rais wa Zanzibar alisema hayo wakati alipokuwa akihitimisha mjadala wa Taarifa ya Utekelezaji wa Mpangokazi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ katika kikao kilichofanyika jana Ikulu.
Alisema wakuu wa Mikoa na Wilaya ndio wenye dhamana katika Mikoa na Wilaya hivyo wanawajibika kwa matokeo yeyote ya utendaji kazi katika Mikoa na Wilaya zao.
“simamieni shughuli zenu kwa kuwasimamia watumishi walio chini yenu na ni lazima kufanya hivyo ili wasifike wakati wakajiona kuwa wao ni watu wasioguswa na wasiohojiwa”aliewaleza viongozi hao na kuongeza kwa kusisitiza kuwa “’performance’ ya Mkoa ni Mkuu wa Mkoa na hivyo hivyo kwa Wilaya ni Mkuu wa Wilaya”
Dk. Shein alisisitiza kuwa Ofisi hiyo ni Ofisi muhimu yenye majukumu makubwa yanayogusa maisha ya kila siku ya wananchi hivyo kuimarisha utendaji na uwajibikaji katika ngazi za mikoa na wilaya ni suala la kipaumbele ili kukidhi matarajio ya wananchi kwa Serikali yao.
Katika mnasaba huo aliwataka wakuu wa Mikoa na Wilaya kufuatlitia kwa karibu kila kitu kinachofanyika katika Ofisi zao na mikoa na wilaya wanazoziongoza na kujiweka tayari wakati wote kujibu hoja za wananchi.

No comments:

Post a Comment