TANGAZO


Sunday, May 18, 2014

Raia wa Uchina wajeruhiwa Vietnam



Waandamanaji wanaopinga Uchina nchini Vietnam

Shirika rasmi la habari nchini Uchina Xhinua limesema kuwa serikali imewaondoa zaidi ya raia wake 3000 kutoka nchini Vietnam kufuatia ghasia dhidi raia wa Uchina nchini humo.
Wafanyikazi wawili wa Uchina wameuawa kufuatia ghasia hizo zilizosababishwa na hatua ya Uchina kupeleka meli yake ya kuchimba mafuta katika eneo linalozozaniwa kusini mwa bahari ya Uchina.
Serikali mjini Beijing inaandaa safari nyingine za ndege huku naibu waziri wa maswala ya kigeni Liu Jianchao akizuru Vietnam kwa mazungunmzo na mamlaka.Mapema hii leo takriban raia 16 wa Uchina waliojeruhiwa vibaya waliondoshwa nchini humo kupitia usafiri wa ndege maalum.
Aidha waziri huyo amewatembelea baadhi ya raia wa Uchina waliojeruhiwa hospitalini.
Wanaharakati nchini Vietnam wameitisha maandamano zaidi dhidi ya raia wa Uchina hii leo licha ya mwito wa serikali wa kutaka kusitishwa kwa maandamano hayo.

No comments:

Post a Comment