TANGAZO


Wednesday, May 14, 2014

Oscar Pistorius kuchunguzwa kiakili


Pistorius amekana madai ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp
Jaji katika kesi ya mauaji ambapo mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius, anashitakiwa kwa kumuua mpenzi wake, ameamuru mwanariadha huyo apelekwe katika kituo cha afya kufanyiwa uchunguzi wa kiakili.
Mnamo Jumatatu, Daktari Bingwa wa akili, aliambia Mahakama kuwa Bwana Pistorius anaugua maradhi yanayaohusiana na kuhangaika.
Jaji alisema kuwa ameridhika kwamba mtaalamu huyo ameshawishi mahakama kuruhusu mshitakiwa kwenda kufanyiwa uchunguzi, ingawa hatua hiyo itachelewesha kuendelea kwa kesi hiyo.
Alisema hatua hiyo hiyo itahakikisha kwamba mshtakiwa anapata haki katika kesi hiyo.
Shahidi mtaalamu - aliyeitwa na upande wa mashitaka - alisema kukatwa miguu yake yote miwili inamweka Pistorius katika hali ambapo akikumbana na tishio atalazimika kujitetea badala ya kutoroka.
Mwanariadha huyo amekiri kumpiga risasi mpenzi wake, Reeva Steenkamp, baada ya kumdhania kuwa jambazi.

No comments:

Post a Comment