TANGAZO


Sunday, May 18, 2014

Mafuriko yakumba mataifa ya Balkan



mafuriko
Juhudi za kuyadhibiti mafuriko mabaya zaidi ambayo yamewaathiri maelfu ya raia wa mataifa ya Balkan zinaendelea.
Mto wa Sava tayari umevunja kingo zake katika miji mingi na sasa ni tishio kwa kiwanda kikubwa cha umeme nchini Serbia.
Mamlaka imesema kuwa kuudhibiti mto huo ndio swala litakalopewa kipaumbele,lakini ikaongezea kuwa usaidizi kutoka nje utahitajika ili kuimarisha juhudi za uokozi.
Maeneo mengi yanayopakana na taifa la Bosnia yako chini ya maji na mafuriko hayo pia yameathiri Croatia.
Zaidi ya watu 20 wanahofiwa kupoteza maisha yao lakini idadi hiyo ianatarajiwa kupanda baada ya maji kupwa.

No comments:

Post a Comment