Shule hii ndio waliokuwepo wasichana hao waliotekwa
Mwanaharakati mwanamke aliyekuwa
akiongoza maandamano nchini Nigeria kushinikiza serikali ya nchi hiyo
kuwaokoa wasichana 200 waliotekwa hivi karibuni ametiwa mbaroni na
polisi kwa amri ya mke wa Rais wa nchi hiyo.
Naomi Mutah Nyadar alikuwa miongoni wanawake
waliohudhuria mkutano ulioitishwa na ma mke wa rais Patience Jonathan na
baadae mwanaharakati huyo alipelekwa kituo cha polisi habari zinasema.Inasemekana Mke wa Rais Jonathan anahisi mama za wasichana waliotekwa walimtuma mwanaharakati huyo ili aweze kuwawakilisha.
Mke wa Rais wa Nigeria Patience Jonathan
Mama Mutah mwakilishi wa jamii ya Chibok eneo ambalo wasichana hao walipotekwa wakiwa shuleni zaidi wiki mbili zilizopita, wiki iliyopita aliandaa maandamano katika mji mkuu wa Abuja.
Waandamanaji wengi wakiwa ni Wanaigeria wanaona serikali ya nchi hiyo haijafanya vya kutosha kuwatafuta wasichana hao waliotekwa wanaodhaniwa kuwa ni kundi la kiislam la Boko Haram.
Hadi sasa Boko haram hawajasema lolote kuhusu tuhuma hizo.
Wasichana wanne walio mbele ambao ni miongoni mwa waliotekwa na kufanikiwa kutoroka
No comments:
Post a Comment