Jeshi Nigeria: twajua waliko wasichana
Jeshi nchini Nigeria linasema
kuwa linajua wanakozuiliwa zaidi ya wasichana 200 waliotekwa nyara
majuma sita yaliyopita lakini likasema haliwezi kutumia nguvu
kuwakomboa.
Afisa wa cheo cha juu jeshini - Mkuu wa Jeshi
Alex Badeh - aliwaambia waandamanaji jijini Abuja kuwa hangeweza
kufichua waliko wasichana hao lakini akaahidi kuwa wanajeshi
watawarejesha nyumbani wasichana hao.
"Habari nzuri kwa wasichana ni kuwa
tunafahamu waliko lakini hatuwezi kuwambia. Hatuwezi kuja na kuwambia
siri za kijeshi hapa," mkuu wa wanahewa Alex Badeh aliwambia
waandamanaji jijini Abuja.
Alisema anaamini kuwa watawarudisha wasichana hao nyumbani hivi karibuni lakini akaeleza masikitiko yake kwa kile alichosema watu kutoka nje ya nchi wanaochochea ghasia na maandamano.
Bwana Badeh alisisitiza kuw kutumia nguvu kujaribu kuwakomboa wasichana hao ni hatari.
"Wapiganaji hawa wanataka kupigana na kwa hivyo wasichana watakuwa hatarini ikiwa kutatokea mkabiliano makali kati ya wapiganaji hao na jeshi la Nigeria," Alex Badeh alisema.

No comments:
Post a Comment