Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Taasisi ya Afya na Tiba Shirikishi Muhimbili (MUIAHSSO), Stephano Haule, akifafanua jambo wakati wa mkutano huo, na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua habari zilizokuwa zikitolewa na Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Taasisi ya Afya na Tiba Shirikishi Muhimbili (MUIAHSSO), Stephano Haule, wakati alipokuwa akizungumza nao, Dar es Salaam leo.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa katika mkutano huo na Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Taasisi ya Afya na Tiba Shirikishi Muhimbili (MUIAHSSO), Stephano Haule pamoja na viongozi wengine wa Serikali hiyo, Dar es Salaam leo.
Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Taasisi ya Afya na Tiba Shirikishi Muhimbili (MUIAHSSO), Stephano Haule (katikati), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kuomba kurejeshwa kwa ada ya zamani kwa wanafunzi wa Cheti na Diploma wa chuo hicho, kinachoendeshwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Kulia ni Waziri Mkuu wa MUIAHSSO, Bosco Sombela na kushoto ni Makamu wa Rais wa MUIAHSSO, James Yohana.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua habari zilizokuwa zikitolewa na Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Taasisi ya Afya na Tiba Shirikishi Muhimbili (MUIAHSSO), Stephano Haule, wakati alipokuwa akizungumza nao, Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua habari zilizokuwa zikitolewa na Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Taasisi ya Afya na Tiba Shirikishi Muhimbili (MUIAHSSO), Stephano Haule, wakati alipokuwa akizungumza nao, Dar es Salaam leo.
AWALI YA YOTE TUNAPENDA KUTAMBUA UWEPO WENU,NA KUTOA
SHUKRANI ZA DHATI KWA MWITIKIO WENU WA KUJA KUTUSIKILIZA,
PIA TUNATOA SHUKRANI ZA DHATI KWA MKURUGENZI WA IDARA YA
MAELEZO KWA KUTUPA KIBALI CHA KUFANYA
MKUTANO HUU WA LEO KATIKA UKUMBI HUU.PAMOJA NA WAFANYAKAZI WOTE WA IDARA
HII YA MAELEZO.
UTANGULIZI
Tunatoa pongezi kwa wanataaluma wote wa habari Tanzania kufanikisha kwa kiasi
kikubwa kuibua na kuleta suluhisho kwa changamoto mbali mbali zinazolikumba
Taifa letu.Pamoja na magumu mnayokumbana nayo bado dhamira yenu ya kulikomboa
Taifa Inasonga mbele.Ninawapongeza sana.
Tumekuja leo hii kwa lengo kuu moja mtusaidie kufikisha Kwa haraka zaidi hatari hii kwa Wadau
muhimu waliopo katika mamlaka mbali
mbali husika,
(a)
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
(b)
Wabunge wote wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania.
(c)
Wizara ya afya na ustawi wa jamii
(d)
Watanzania wote wajue hatima ya nchi yao kwani ndio
wanaowachagua wawakilishi wao kwenda kutetea haki zao katika chombo muhimu cha
Bunge.
(e)
N.k
Serikali ya wanafunzi kupitia Rais wake iliandika nyaraka za
barua kadhaa kutoa tahadhali hii,lakini hadi sasa zimebakia siku chache tu Kwa
Bajeti ya Wizara ya Afya kusomwa Bungeni,ahadi tu zimesalia tutawatumia majibu
kwa njia ya barua.
HITIMISHO
Ni hatari kubwa kuona vyombo na mamlaka muhimu nchini
zikifanya mzahaa na Maisha ya Watanzani.
Tunatambua wazi “hakuna haki inayoweza kuja kama zawadi”
Hivyo Serikali ya wanafunzi (MUIAHSSO) ,wanafunzi
,ikishirikiana na vyuo vyote vya afya Nchini husika na janga hili la kitaifa na
Wananchi wote wa Tanzania,endapo Muhimili huu Muhimu wa Bunge utashindwa kuleta
suluhisho wakati Bajeti ya Wizara Ya Afya ikipitishwa na kuacha Watanzania
katika hatari hii.
Tutatambua wazi kwamba hata wawakilishi wetu tuliowapigia
kura wakatutetee bungeni wametugeuka na kuamua kuisaliti Nchi Yetu na
kulipeleka Taifa katika giza nene.
Hivyo Watanzania
katika hili hatutaweza kuvumilia hata kidogo hatua Muhimu zitachukuliwa
ikiwamo:-
(A)
Maandamano ya amani kuomba Serikali Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Ijihuzuru,Endapo
haitakuwa na suluhisho la hatari hii.
(B)
Wabunge wote wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania wajihuzuru, Endapo watashindwa kuziwajibisha mamlaka husika.
Narejea kauli za Baba wa Taifa Letu Mw.J.K Nyerere “Endapo
mtu yeyote hana uchungu na umasikini
tulionao hatufai hata kidogo” Wale wanaoungalia utajiri wao hatuna budi
kuwang’oa kwa gharama yoyote ile kwa ukombozi wa taifa letu
MUHIMBILI UNIVERSITY


(MUIAHSSO)
P.O.BOX 65005, DAR ES SALAA M.
KWA NIABA YA
WATANZANIA WOTE

20/01/2014.
Kumb.Na.MUIAHSSO/EXCOM/TANZANIA./VOL.1
KATIBU MKUU,
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII,
S.L.P 9083.
DAR ES SALAAM.
Ndugu,
YAH:HALI YA HATARI KWA WATANZANIA WA KIPATO CHA
CHINI KUKOSA KABISA FURSA
YA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA AFYA KATIKA NGAZI YA CHETI (CERTIFICATE) NA
STASHAHADA (DIPLOMA)
Rejea kichwa hapo juu,
Kuna hatari kubwa ya watanzania wengi wa
kipato cha chini kushindwa kujiunga na mafunzo ya fani za afya katika ngazi ya
Cheti (certificate) na stashahada (diploma) kutokana na ongezeko kubwa la
gharama za uchangiaji katika vyuo vya mafunzo ulioanza kwa kasi katika mwaka wa
masomo wa 2012/2013.
Rejea barua ya kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya
yenye Kumb.Na. JC.166/235/01‘A’/210 aliowaandikia wakuu wa vyuo vya
afya Tanzania Bara, Tarehe 19 July,2012.
Nanukuu “kutokana na
kuongezeka kwa gharama za uendeshaji wa vyuo na bajeti kuwa finyu kila mwaka
Wizara imefikia uamuzi wa kuongeza viwango vya gharama za uchangiaji”
Barua hii ilitoa mwanya
wa michango mingi kuongezeka.Baadhi ya vyuo ongezeko lilikuwa zaidi ya asilimia
111.9 (111.9%),160.6& na vingine ongezeko
lilikuwa zaidi ya asilimia
174.(174%).kutoka gharama za awali.
Rejea na barua nyingine ya tarehe 04/11/2013, Yenye
Kumb.Na.JB 425/558/03E/27.Nanukuu “Kutokana na kuongezeka kwa gharama ya uendeshaji wa mafunzo na
upungufu wa bajeti
ya serikali, Wizara imeongeza viwango vya gharama za uchangiaji”.
Mlitumia njia hii ya kuongeza gharama kwa wanafunzi ili kunusuru
uendeshaji wa vyuo ni jambo jema,lakini tatizo lilikuwa ni ufinyu wa bajeti na
gharama za uendeshaji kuongezeka na matokeo yake bajeti inazidi kuwa finyu kila
mwaka na gharama za uendeshaji zinazidi kuongezeka kila mwaka,hali inayozidi
kumbebesha gunia la misumari mtanzania wa hali ya chini asiyeweza kumudu
gharama hizi kushindwa kupata haki yake ya msingi ya kupata elimu ili aje
alitumikie taifa lake.
Naiomba wizara ifikiri
zaidi. Utatuzi wa tatizo la gharama kwa kuongeza gharama kubwa kwa wanafunzi
itapelekea kukosa wataalamu wazuri ambao wanashindwa kujiunga na mafunzo kwa
kukosa pesa.Na kama pesa itazidi kuwa ni kigezo cha kupata elimu tutambue wazi
siku za usoni tutakuwa na upungufu
mkubwa wa wafanyakazi wa afya vijijini.
Mnatambua wazi utendaji
na umuhimu wa wataalamu hawa wa afya (both certificate and diploma).Katika
kuokoa maisha ya watanzania.
Hivyo naishauri wizara
itafute mbinu nyingine mbadala ili kunusuru janga hili.
a) Kupitia upya vigezo vilivyotumika kupandisha gharama
ukilinganisha na kipato halisi cha mtanzania.(kipato cha mzazi au mlezi)
b) Wizara ikishirikiana na mamlaka husika uanzishwe mfumo
wa wanafunzi kupata mkopo kutoka Bodi ya mikopo kama ilivyo kwa wanafunzi wa
Shahada endapo hoja ya kuwapunguzia watanzania gharama za uchangiaji inapata
kigugumizi.
c) Kurudisha vyuo vyote fya wizara ya afya kuendeshwa na
serikali (Wizara) kwa maslahi ya watanzania wote.kuruhusu kwa baadhi ya vyuo
kujiendesha ni kuwaumiza watanzania.
d) Kuvunja mifumo yote inayopelekea mali za umma kutumika
kwa maslahi binafsi pasina kuwafikia walengwa.
Tupo tayari wakati wowote
tutakapohitajika kushirikiana na wizara
kutafuta suluhu ya kudumu itakayotoa matumaini mapya kwa Watanzania juu
ya hoja hii.Kwa ustawi wa taifa na afya za Watanzania.
Waraka huu hauna lengo
lolote la kulaumu mamlaka yoyote,ni kwa nia njema ya kutafuta suluhu ya hoja
hii kwani ongezeko hilo lilikuwa ni kwa nia njema ya kuendesha vyuo.Kwa bahati
mbaya hali halisi ya maisha ya watanzania ni changamoto ngumu sana kwao kumudu
gharama hizo.Hivyo serikali ina kila sababu ya kuhakikisha wananchi wake
wanapata elimu kwa kutumia rasilimali tulizonazo nchini.
Wako katika ujenzi wa
taifa
Stephano Haule
Rais wa Serikali ya
wanafunzi(MUIAHSSO) .
Simu namba:0715695619


(MUIAHSSO)
P.O.BOX 65005, DAR ES SALAA M.
KWA NIABA YA
WATANZANIA WOTE

20/01/2014.
Kumb.Na.MUIAHSSO/EXCOM/TANZANIA./VOL.1
SPIKA WA BUNGE,
BUNGE LA JAMUHURI YA MUUNGANO WA
TANZANIA,
S.L.P 941,
DODOMA.
Ndugu,
YAH:HALI YA HATARI KWA WATANZANIA WA KIPATO CHA
CHINI KUKOSA KABISA FURSA
YA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA AFYA KATIKA NGAZI YA CHETI (CERTIFICATE) NA
STASHAHADA (DIPLOMA)
Husika na kichwa hapo juu.
Mheshimiwa Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kutokana na hatari hii kubwa inayohatarisha hatima ya watanzania walio
wengi kukosa fursa hii kwa kigezo cha kukosa pesa.
Tunakuomba kupitia Bunge lako tukufu.
Rejea kiambatanisho cha
baru barua ya kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Afya yenye Kumb.Na.
JC.166/235/01‘A’/210 aliowaandikia wakuu wa vyuo vya afya Tanzania Bara, Tarehe 19 July,2012.
Nanukuu “kutokana na
kuongezeka kwa gharama za uendeshaji wa vyuo {ngazi ya CHETI(CERTIFICATE) NA
STASHAHADA (DIPLOMA)} na bajeti kuwa finyu kila mwaka Wizara imefikia uamuzi wa
kuongeza viwango vya gharama za uchangiaji”
Rejea kiambatanisho
cha waraka mwingine kutoka wizara ya afya na ustawi wa jamii wa tarehe
04/11/2013, Kumb.Na JB 425/558/03E/27.Nanukuu “Kutokana na kuongezeka kwa
gharama ya uendeshaji wa mafunzo na upungufu wa bajeti
yaserikali, Wizara imeongeza
viwango vya gharama za uchangiaji”.
Naamini Bunge lako tukufu linatambua hali halisi ya kipato cha
Mtanzania.Na ni wazi kwamba watanzania walio wengi wanaishi vijijini katika
maisha duni sana.Fikiria kama kulipa tu ada ya sekondari ameshindwa atapata
wapi uwezo wa kujilipia laki nane,laki tisa au milioni? Na dalili zinazoonekana
hali inazidi kuwa mbaya zaidi kila mwaka.
Rejea kiambatanisho Na.10.cha mfano hai wa baadhi ya chuo kimojawapo
unaoonesha wazi ni jinzi gani waraka huu ulivyopelekea maumivu makali kwa
watanzania. Kutoka (307,000Tshs hadi kufikia 842,400Tshs) Haya yalikuwa ni
mabadiliko ya ndani ya mwaka mmjo tu,na tunakoelekea hali inazidi kuwa mbaya zaidi.
Mpaka sasa tayari kunaongezeko jingine tayari na hali inazidi kuwa mbaya kwa
watanzania. Bunge lako tukufu linatambua wazi hali halisi ya kipato cha
mtanzania.Nimetoa kielelezo hiki ili muone wazi kama kuna usalama wowote kwa
mtanzania wa kipato cha chini.
Baba wa Taifa Mwalimu J.K NYERERE wakati ule anatoa elimu bure
haikumaanisha kwamba hawakuwepo watanzania wenye uwezo wa kulipia watoto wao
ada za shule hapana.Ila alitambua kuwa kuna kundi kubwa la Watanzania
hawataweza kulipa gharama hizo.Akaona iko sababu ya kuwekeza katika elimu.
Mheshimiwa Spika, Taifa lolote ambalo litashindwa kusomesha wananchi
wake,litashindwa kuwekeza katika elimu,litabinafusisha elimu.Huo ndio utakuwa
mwisho wa taifa hilo kuonekana katika ramani ya Dunia.
Mheshimiwa spika, ninakuomba sana kupitia Bunge lako tukufu,kuzuia
maongezeko holela ya gharama za mafunzo katika vyuo vyote vya afya Tanzania na
kutangaza rasmi mpango madhubuti wa serikali kupitia bunge lako tukufu hatima
ya kuwaokoa watanzania katika mashua hii itakayozamisha wanyonge wengi
Mheshimiwa spika, Mwalimu J.K Nyerere Baba wa Taifa letu alisema maneno
haya “HAKUNA KULA MBEGU WAJINGA WANAKULA MBEGU” kwa ukombozi wa Tanzania dhidi
ya maadui wakuu watatu (UJINGA,UMASIKINI Na MARADHI) njia pekee ni kupanda
MBEGU katika elimu,mavuno yake yataleta faraja kubwa katika taifa letu.
Mheshimiwa spika Mwalimu alisema “KWA WENYE NGUVU KUUNGANA KWAO NI
UPUUZI”Hawataki kabisa kusikia wanyonge wakiungana kwasababu itakuwa ndio
mwisho wao, na akasema maneno haya ”WAKATI WENYE NGUVU WANAUNGANA KUWAKANDAMIZA
WANYONGE, WANYONGE WANAGOMA KUUNGANA”
Mheshimiwa spika,wapo watu wachache ambao hawataona umuhimu wa
tahadhari hii hata kidogo na kutafuta namna ya kuzifisha harakati hizi kwa
makusudi kwa kuwa wana maslahi binafsi.Wapo waliojilimbikizia mali,wanaoibia
umma wanatambua kwamba kama wataruhusu mwanya huu kupenya na watu wenye uchungu
na nchi yao wakapata elimu ya kutosha watageuka kuwa mwiba kwa maovu yao.
Mheshimiwa spika,tunaomba katika Bunge lijalo mjadili hoja hii kwa umakini
ili kuleta ahuweni kwa watanzania kwani wanaoumia si wanafunzi tu bali pia
wazazi na walezi ambao wanategemea sana kutetewa na muhimili huu muhimu.
Ikishindikana kupunguza gharama hizo
basi ni wakati mwafaka kuingiza wanafunzi wa mafunzo haya katika mfumo
wa kulipiwa na Bodi ya mikopo.Kama
ilivyo kwa elimu ya juu (shahada)
Mheshimiwa spika naishauri serikali kupitia bunge lako tukufu itoe
miongozo itakayodhibiti upandaji wa gharama katika vyuo vya umma kwa
kushirikisha wadau wote pamoja na wanafunzi.Wanafunzi wakishirikishwa vema
katika mazingira ya uwazi na ukweli italiwezesha taifa kuokoa mabilioni ya pesa
ya serikali yanayopotea kupitia watumishi wa umma wasiokuwa waadilifu.
MADHARA KWA TAIFA
a) Kukithiri kwa vitendo vya kihalifu
(rushwa,ujambazi,uuzaji na utumiaji madawa ya kulevya)
b) Inatengeneza matabaka makubwa kwa aliyekuanacho na
asiyekuanacho.
c) Itapelekea miaka michache ijayo taifa kutotawalika
kutokana na chuki itakayoibuka miongoni mwa matabaka (VITA VYA WENYEWE KWA
WENYEWE)
d) Kukosekana kwa uadilifu kwa watumishi wa umma.Mshahara
anaoupata mzazi au mlezi hautoshelezi kumpeleka shule mtoto hivyo atalazimika
kutumia nafasi aliyonayo kinyume na maadili kujiongezea pesa ili aweze
kusomesha watoto.Kupitia Bunge lako tukufu mnatambua hali halisi ya maisha na kipato cha wazazi na walezi.
e) Upungufu mkubwa wa wataalamu wa afya waadilifu siku za
usoni.
Ni matumaini ya
watanzania kuwa bunge lako tukufu litalishughulikia Hoja hii mapema sana,Tunaamini
Bunge lijalo hoja hii itajadiliwa na kupata mwafaka ambao utapelekea mabadiliko
makubwa katika bajeti ijayo.
Sisi vijana wenu
tunaipenda sana nchi yetu na tunaahidi kushirikiana bega kwa bega kutafuta
suluhu za changamoto zinazolikumba taifa letu,nakusaidiana kutafuta namna
ambayo itaijengea heshima kubwa nchi yetu kuwa kisiwa cha amani miaka yote.
Nimeambatanisha nakala
ya barua niliyomwandikia Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na mamlaka zote husika.
Wako katika ujenzi wa
taifa
Stephano Haule
Rais wa Serikali ya
wanafunzi(MUIAHSSO) .
Simu namba:0715695619


(MUIAHSSO)
P.O.BOX 65005, DAR ES SALAA M.
KWA NIABA YA WATANZANIA
WOTE

20/01/2014.
Kumb.Na.MUIAHSSO/EXCOM/TANZANIA./VOL.1
JUKWAA LA WAHARIRI
VYOMBO VYA HABARI
Ndugu,
YAH:HALI YA HATARI KWA WATANZANIA WA KIPATO CHA
CHINI KUKOSA KABISA FURSA
YA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA AFYA KATIKA NGAZI YA CHETI (CERTIFICATE) NA
STASHAHADA (DIPLOMA)
Wahariri vyombo vya
habari.
Kupitia taaluma yenu tunaomba mtusaidie kufanya tathmini vijijini,
mijini, Kwa wakulima, wafanyakazi n.k.Muone hali halisi Na nini hatima ya
Tanzania ya kesho katika elimu,mtusaidie kutufikishia hoja hii kwa viongozi
husika na wawakilishi wetu Bungeni.Tuliokoe taifa letu la Tanzania.Miaka 50
ijayo wajukuu wetu waimbe wimbo wa “Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo
wote……………..”kwa furaha tutakayoipanda leo kwa umoja kwa Taifa kuwekeza katika
elimu
Hoja hii nimeitolea maelezo katika viambatanisho vya nakala za Barua
kwa Katibu MKuu Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii na nakala ya Barua
niliyomwandikia Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania.
Wako katika ujenzi wa taifa
Stephano Haule
Rais wa Serikali ya
wanafunzi(MUIAHSSO) .
Simu namba:0715695619


(MUIAHSSO)
P.O.BOX 65005, DAR ES SALAA M.
KWA NIABA YA
WATANZANIA WOTE

20/01/2014.
Kumb.Na.MUIAHSSO/EXCOM/TANZANIA./VOL.1
MWEYEKITI,
TUME YA HAKI
ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA,
Box 2643
Ndugu,
YAH:HALI YA HATARI KWA WATANZANIA WA KIPATO CHA
CHINI KUKOSA KABISA FURSA
YA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA AFYA KATIKA NGAZI YA CHETI (CERTIFICATE) NA
STASHAHADA (DIPLOMA)
Nanatambua mchango wenu
katika kulinda na kutetea haki za binadamu.
Nchi yetu ya Tanzania
ina maadui wakuu watatu:-
a) Ujinga
b) Umasikini
c) Maradhi
Tunawaomba
mpitie kwa umakini madai yetu,na kutusaidia kuishauri serikali ya Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania ione sababu ya kuweka kipaumbele cha kuwaokoa watanzania
na hawa maadui wakuu watatu hatari ambao
ikiachwa bila kushugulikiwa italiteketeza taifa
Nimeambatanisha
na maelezo ya hoja hii katika nakala za barua kwa Kwa Katibu Mkuu Wizara ya
Afya na nakala ya Barua niliyomwandikia Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania.
Wenu katika utetezi wa
haki za binadamu,
Stephano
Haule
Rais
wa serikali ya wanafunzi (MUIAHSSO)
Namba
ya simu:0715695619
Kumb.Na.MUIAHSSO/EXCOM/TANZANIA./VOL.1
Nakala kwa:-
1. WAZIRI MKUU WA SERIKALI YA JAMUHURI YA MUUNGANO YA
TANZANIA.
2. SPIKA WA BUNGE LA JAMUHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA.
3. WAZIRI WA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII.
4.
WAZIRI
KIVULI WA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII (KAMBI YA UPINZANI BUNGENI).
5. KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII.
6. MKURUGENZI WA MAFUNZO WIZARA YA AFYA.
7. JUKWAA LA WAHARIRI VYOMBO VYA HABARI TANZANIA.
8. MWEYEKITI TUME
YA HAKI ZA BINADAMUNA UTAWA BORA.
9.
WALEZI WA
WAWAFUNZI TAASISI YA AFYA NA TIBA-CHUO KIKUU CHA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI
MUHIMBILI.
KIAMBATANISHO
NAMBA 10
MFANO
HAI WA MABADILIKO YALIYOTOKEA NDANI YA MWAKA MMOJA TU kwa moja ya chuo cha
wizara ya afya ikiwa ni matokeo ya barua
ya kaimu katibu mkuu wizara ya afya kwa wakuu wa vyuo.2011/2012,ILIKUWA LAKI
TATU NA SABA elfu tu (307,000Tshs).
Mwaka
wa masomo 2012/2013,ilipanda hadi kufikia laki nane arobaini na mbili elfu na
mia nne.(842,400Tshs) (for Government sponsored Students)
Ongezeko
hilo lilikuwa zaidi ya asilimia mia moja sabini na nne ( more than174%)kutoka
gharama za awali.
No comments:
Post a Comment