Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ameahidi Uingereza "kufanya kile itakachoweza" kusaidia kuwapata wasichana wa shule zaidi ya 200 waliotekwa na magaidi wa Boko Haram.
Wapiganaji wa Kiislam wa kikundi cha Boko Haram wamedai kuhusika na utekaji wa wasichana hao.
Wakati wa programu hiyo ya BBC, mgeni mwaalikwa Christiane Amanpour, mwandishi wa habari mkuu wa kimataifa wa CNN, alimkabidhi bwana Cameron karatasi lenye maandishi ya "#Bring Back Our Girls" na kumwuliza kama angependa kujiunga na kampeni hiyo.
Baadaye Bwana Cameron alituma ujumbe kwa njia ya tweeter: "Ninafuraha kuunga mkono kampeni ya #BringBackOurGirls."
Waziri mkuu huyo wa Uingereza alikiambia kipindi cha BBC One programme: "nilimpigia simu rais wa Nigeria kusaidia chochote ambacho kingwezesha kupatikana kwa wasichana waliotekwa na tumekubaliana kutuma timu ya wataalam wakiwemo wa kukabiliana na vitendo vya ugaidi na ujasusi ili kufanyakazi kwa pamoja na timu kubwa ya wataalam wa Marekani wanaokwenda huko.
"Tuko tayari kufanya lolote zaidi ambalo Wanigeria watataka tufanye."
Amesema huenda Nigeria isiombe msaada wa majeshi ya Uingereza lakini amesema: "Nimemwaambia Rais Jonathan, pale tutakapoweza kusaidia, tafadhali aseme, na tutaona tukachoweza kusaidia."
Mke wa Rais wa Marekani, Michelle Obama amekuwa akipiga kampeni ya kuachiliwa kwa wasichana waliotekwa.
"Hili si tatizo tu la Nigeria," amesema. "Kwa kweli tunaona misimamo hii mikali ya Uislam- tunaona matatizo Pakistan, tunaona matatizo katika maeneo mengine ya Afrika, matatizo Mashariki ya Kati.
"Pia, hebu tu wakweli, hapa Uingereza bado kuna vikundi vyenye kuunga mkono misimamo mikali ya kidini, ambayo tunatakiwa kukabiliana nayo, iwe mashuleni, vyuoni au vyuo vikuu na kwingineko.."
Anaelewa kuwa si kazi rahisi kuwatafuta wasichana, ambao walitekwa kutoka shuleni kwao Chibok tarehe 14 Mei 2014 katika jombo la Borno.
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis pia naye ametuma ujumbe wa tweeter akiunga mkono kampeni ya kurejeshwa wasichana hao akiandika: "tuungane katika maombi ili kuachiliwa haraka kwa wanafunzi hao wa kike waliotekwa nchini. #BringBackOurGirls."
No comments:
Post a Comment