TANGAZO


Tuesday, April 8, 2014

Wadau wa filamu nchini waaswa kuendelea kupeperusha bendera ya Tanzania

Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi Joyce Fisoo akieleza lengo la kikao cha wadau wa filamu ni pamoja na kujadili masuala ya maendeleo ya tasnia ya filamu nchini na mapendekezo ya wadau kuhusu bodi ya filamu kuitisha mjadala wa wazi wa wadau wa filamu hususani wasambazaji, waandishi wa miswada na watayarishaji ili kujadili masuala mbalimbali yanayohusu tasnia hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akitoa hotuba ya ufunguzi wa kikao cha wadau wa filamu kuhusu mustakabali wa soko la filamu nchini leo, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa filamu walioshiriki kikao cha kujadili masuala mbalimbali ya husuyo tasnia hiyo leo jijini Dar es salaam. Pichani ni wasanii wa “Bongo Movie” (wa kwanza kushoto ni Steven Mengele “Manyerere”, Emmanuel Muyamba (katikati) na wa kwanza kulia ni Jacobo Steven “JB”.
Picha ya pamoja ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga (wa sita kutoka kushoto mstari wa mbele) baada ya ufunguzi wa kikao cha wadau wa filamu kuhusu mstakabali wa soko la filamu nchini leo jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

No comments:

Post a Comment