Wapiganaji nchini Sudan kusini wanasema wameudhibiti mji mkubwa
katika jimbo lenye utajiri wa mafuta, na wametoa makataa kwa makampuni ya mafuta
kusitisha utengenezaji wa mafuta na iwaondoshe wafanyakazi.
Walinda amani wa Umoja wa mataifa waliwaokoa wafanyakazi kumi wa kampuni ya
mafuta ya Urusi, Safinat kaskazini mwa mji wa Bentiu, kutoka ghasia hizo, watano
kati yao walijeruhiwa.Akizungumza kwa njia ya simu kutoka jimbo la Unity, kamanda mmoja wa waasi alieleza kwamba kikosi cha waasi kimeudhibiti upya mji wa Bentiu kutoka kwa wanajeshi wa serikali.
Athari za ghasia
Sudan kuisni imeshuhudia ghasia kubwa mnamo mwezi Desemba, wakati kulizuka mapigano kati ya wanajeshi wanaomtii aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar na wale wanaomtii rais Salva Kiir.
Maelfu ya watu wanaaminika kuuawa huku wengine zaidi ya milioni wakiyakimbia makaazi yao.
Amesema kuzuka upya mapigano hayo kutaathiri jitihda za kuepuka baa la njaa linalotarajiwa.
Maafisa wa mashirika ya kimataifa ya misaada wametumia 'baa la njaa' mara kwa mara kuelezea hali itakayoikabili Sudan kusini katika miezi ijayo.
Nchi hiyo ni maskini na wakaazi wengi wanaishi kwa kula vyakula wanavyopanda na kuvuna. Kutokana na mapigano yanayoendelea, wakaazi wengi wanashindwa kupanda vyakula kwa matayarisho ya msimu ujao wa mvua.
No comments:
Post a Comment