Viongozi wa mashitaka nchini Korea Kusini wameiomba mahakama
kutoa kibali cha kukamatwa kwa nahodha wa feri ya abiria iliyozama siku ya
Jumatano ikiwa imewabeba zaidi ya watu 400.
Hadi kufikia sasa watu mia mbili na sabini hawajulikani waliko.Mmoja wa wapiga mbizi hao alisema kuwa hawakufanikiwa kuiona vizuri feri hiyo hali iliyowalazimu kuiguza kwa mikono yao.
Afisa wa ulinzi wa pwani Ko Myung Suk amesema kuwa hawakupata manusura yeyote eneo walilofanikiwa kufika
Naibu mwalimu mkuu kwenye shule ambapo wengi wa wanafunzi walikuwa wakisomea amepatikana ameaga dunia.
Vyombo vya habari vinasema kuwa huenda mwalimu huyo amejitoa uhai.
No comments:
Post a Comment