TANGAZO


Thursday, April 10, 2014

Timu ya watoto wa mitaani kutoka Tanzania iliyoibuka mabingwa wa dunia yapokelewa kishujaa

Mwenyekiti wa Timu ya watoto wa mitaani ya jijini Mwanza, Alfat Mansoor (Dogo), akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya timu hiyo kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana, jijini Dar es Salaam.
Mchezaji aliyesabibisha timu ya watoto wa mitaani kutoka Tanzania kuibuka mabingwa wa Dunia kwa kufunga magoli matatu kwa moja dhidi ya Burundi, Frank William (mwenye kofia nyekundu), akiwa na baadhi ya wachezaji wenzake mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa  Kimataifa wa Mwalimu Julius Shirikisho. Kushoto ni Hassan Jaffar, Emmanuel Amos na Hassan Seleman.
Mkurugenzi  Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo, Bi. Juliana Yassoda akiwa amebeba kombe la ubingwa wa dunia mara baada ya kupokea timu ya watoto wa mitaani kutoka Tanzania iliyochukua ubingwa huo kwa kuifunga timu kutoka Burundi jumla ya magoli 3-0. Timu hiyo imewasili nchini jana majira ya saa 9:35 mchana na kulakiwa na uongozi wa Serikali na wadau mbalimbali wa soka.
Wachezaji wa timu ya watoto wa mitaani ya Tanzania iliyonyakuwa ubingwa wa dunia katika mashindano yaliyofanyika nchini Brazil kwa kushirikisha timu za watoto wa mitaani, wakiwa wamebeba makombe waliyoyapata  katika mashindano hayo.
Ofisa Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Frank Shija akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji wa timu ya watoto wa mitaani. (Picha zote na Frank Shija, Ofisa Mawasiliano Serikalini, WHVUM)

No comments:

Post a Comment