TANGAZO


Thursday, April 10, 2014

Taasisi ya WAMA na China washirikiana kuisadia jamii nchini

Mkurugenzi wa Uboreshaji Afya wa Wama, Dk. Sarah Maongezi (kulia) akiongea na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam, kuhusu ushirikiano uliopo baina ya Taasisi ya Wanawake na Maendeleo pamoja na Jamhuri ya watu wa China nchini katika kusaidia wananchi, ikiwemo ziara wanayo tarajia kuifanya katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, kuanzia tarehe 12 hadi 19 Aprili, mwaka huu. Katikati ni Katibu wa Balozi wa China nchini, Ren Zhihong na Meneja Mawasiliano wa Wama Philomena Marijani.
Katibu wa  Balozi wa Jamuhuri ya watu wa China nchini, Ren Zhihong (katika) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano uliofanyika maelezo leo jijini Dar es salaam kuelezea ushirikiano uliopo baina ya Taasisi ya Wama na Ubalozi wa China katika shughuli za kusaidia jamii. Kulia ni Mkurugenzi wa Uboreshaji Afya Wama ,Dkt.Sarah Maongezi na kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Wama Philomema Marijani. (Picha na Lorietha Laurence)


Na Lorietha Laurence
Taasisi ya Wanawake na Maendeleo  kwa kushirikiana na Balozi wa Jamuhuri  ya watu wa china nchini, Lu You Qing  itafanya ziara kuitembelea Mikoa ya Kanda ya ziwa kuanzia tarehe 12 hadi 19 Aprili, mwaka huu kwa  shughuli za kusaidia jamii.

Akiongea na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Uboreshaji Afya, Dk. Sarah Maongezi.

Maongezi amesema lengo la ziara hiyo ni kusaidia jamii za watu wa kanda ya ziwa katika sekta za afya, elimu pamoja na kuwawezesha wanawake kujikwamua kiuchumi.

“Lengo kuu la ziara hii ni kuwasaidia wananchi wa Mikoa ya Mara, Simiyu, Kagera na Kigoma kwa kutoa huduma ya afya na elimu bure pamoja na kuwasaidia wanawake waweze kujiinua kiuchumi ili kuimarisha ushirikiano wa shughuli za maendeleo na uwekezaji”, alisema Dk. Maongezi.

Aliongeza kuwa shughuli zitakazofanywa katika ziara hiyo ni kuwatambulisha  wataalamu wa afya kutoka China, ambao watatoa huduma ya upimaji wa afya na dawa  bure katika Hospitali ya Wilaya ya Butima, na msaada ya vyerehani kwa vikundi vya wanawake wajisiriamali pamoja na vitabu, mabegi  na mipira ya kuchezea. 

“Wama haiko kwa ajili ya wanawake na watoto wa kike tu bali inasaidia watu wote, wake kwa waume, kwasababu kila alipo mwanamke na mwanaume naye yupo nyuma yake, hivyo inawahusisha watu wote ingawa imejikita zaidi kwa wanawake.” alisema Dk. Maongezi.

Naye Katibu wa Balozi wa Jamuhuri ya watu wa China nchini Ren Zhihong ameusifu uhusiano mzuri uliojengeka kati ya Serikali ya Jamuhuri ya watu wa China na Tanzania, ulidumu kwa miaka 50 na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo katika shughuli mbalimbali za kijamii.

Taasisi ya Wama, ipo chini ya uongozi wa, mke wa Rais, Mama Salma Kikwete na imejizatiti katika kuwawezesha wanawake na wasichana ili kujenga jamii yenye afya, maendeleo na iliyo elimika, ikisimamia dira ya “Wanawake wa Tanzania wanawezeshwa kuishi maisha bora”.

No comments:

Post a Comment