* Wajumbe wanaosimamia Rasimu kama ilivyowasilishwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, watoka ukumbini
* Wasema ni bora kurudi majumbani kwao kuliko kuwa muhuri wa kupitisha Rasimu mbadala ya CCM
*Nakala za Hati za Muungano zaoneshwa
Na Kassim Mbarouk
WAJUMBE wa Bunge Maalum la Katiba wanaosimamia Rasimu ya Katiba kama ilivyowasilishwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Sinde Warioba, leo jioni wametoka ukumbini mwa Bunge kwa kile walichosema hawaridhishwi na mwenendo wa bunge hilo hasa kutokana na matusi, kejeli pamoja na kuwabagua wananchi kutokana na asili waliyotoka.
Aidha suala ya kukishutumu Chama Cha Mapinduzi kupenyeza Rasimu mbadala na kuipiga teke iliyotayarishwa na tume hiyo na kutoa kejeli kwa wajumbe wa tume nako pia kumepigilia msumari wa kuwatoa kwenye jengo hilo la kutunga katiba mpya inayotegemewa na wananchi.
Lakini pia wameeleza sababu nyingine kuwa ni kwa Waziri waliyemtaja kuwa William Lukuvi kupiga kampeni kanisani akichochea chuki dhidi ya Wazanzibari kuwa wanataka kuanzisha dola ya Kiislamu kwa kudai Serikali 3 kwenye rasimu ya Katiba hiyo, suala walilosema kwamba halikubaliki kwani linaweza kusababisha mauaji kama yale yaliyotokea nchini Rwanda miaka 20 iliyopita.
Aidha mjumbe ambaye ni mmoja wa viongozi wa UKAWA, wanaosimamia kile wanachokiita Katiba ya maoni ya wananchi, Profesa Ibrahim Lipumba, aliponyanyuka kuchangia alizitaja shutuma nyingi dhidi ya njama ya kuuteka mchakato huo na kuingiza kile walichokiita rasimu mbadala ya Chama Cha Mapinduzi jambo alilosema hawakubaliani nalo na kwa hivyo hawatokubali kuwa muhuri wa matakwa ya chama hicho na hivyo kuamua kutoka kwenye ukumbi wa Bunge na kuwaeleza wajumbe kutoka chama hicho kuwa wao hapo ndio mwisho wao kamwe hawatoweza tenda kuendelea na kile walichokiita hadaa ya kuwahadaa wananchi na kutumia fedha nyingi za wananchi kwa walichodai mchezo mchafu unaochezwa na chama hicho kupitia wajumbe wake bungeni humo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho (kushoto) na Ismail Jussa Ladhu, wakizungumza jambo, nje ya ukumbi wa Bunge, baada ya kikao cha kujadili Sura ya Kwanza na ya Sita za Rasimu ya Pili ya Katiba, mjini Dodoma leo. |
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri wa Sheria wa Serikali ya Zanzibar, Aboubakar Khamis Bakar, akichangia Sura ya Kwanza na ya Pili za Rasimu ya Katiba kwenye bunge hilo, mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, wakifuatilia michango ya wajumbe wenzao katika Sura ya Kwanza na ya Pili za Rasimu ya Katiba kwenye bunge hilo, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akichangia Sura ya Kwanza na ya Pili za Rasimu ya Katiba kwenye bunge hilo, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akichangia Sura ya Kwanza na ya Pili za Rasimu ya Katiba kwenye bunge hilo, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Khalifa, akichangia Sura ya Kwanza na ya Pili za Rasimu ya Katiba kwenye bunge hilo, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Khalifa, akichangia Sura ya Kwanza na ya Pili za Rasimu ya Katiba kwenye bunge hilo, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa bunge hilo, Samuel Sitta (kulia), akimsikiliza mjumbe mwenzake, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, walipokuwa wakiteta jambo kwenye kikao hicho leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Thuwaiba Edington Kisasi, akichangia Sura ya Kwanza na ya Pili za Rasimu ya Katiba kwenye bunge hilo, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Ismaili Jussa Ladhu, akichangia Sura ya Kwanza na ya Pili za Rasimu ya Katiba kwenye bunge hilo, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Ismaili Jussa Ladhu, akichangia Sura ya Kwanza na ya Pili za Rasimu ya Katiba kwenye bunge hilo, mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tbaijuka wakizungumza jambo kwenye ukumbi huo, wakati wa kikao hicho.
Mmoja wa wajumbe wa upinzani akichangia vifungu vya Sura hizo.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samia Suluhu Hassan, akiwaonesha wajumbe wa bunge hilo, kopi ya Hati ya Muungano, wakati wa kikao hicho, bungeni humo leo.
Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samia Suluhu Hassan, akiwaonesha wajumbe wa bunge hilo, kopi ya Hati ya Muungano, wakati wa kikao hicho, bungeni humo leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Zitto Kabwe, akichangia Sura ya Kwanza na ya Pili za Rasimu ya Katiba kwenye bunge hilo, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Zitto akichangia umbini humo leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Zitto Kabwe, akichangia Sura ya Kwanza na ya Pili za Rasimu ya Katiba kwenye bunge hilo, mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa bunge hilo, Samuel Sitta (kushoto), Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Anne Makinda (katikati), wakimsikiliza mjumbe mwenzao, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho, walipokuwa wakiteta jambo kwenye kikao hicho leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Zainab Kawawa, akichangia Sura ya Kwanza na ya Pili za Rasimu ya Pili ya Katiba, katika kikao hicho, mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa (kulia) na Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Mrema, wakifuatilia michango iliyokuwa ikitolewa na wajumbe waliokuwa wakichangia kwenye sura hizo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Tundu Lissu akichangia Sura ya Kwanza na ya Pili za Rasimu ya Pili ya Katiba, huku akiwa ameshikilia Katiba za Zanzibar na Tanzania, katika kikao hicho.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akichangia Sura ya Kwanza na ya Pili za Rasimu ya Pili ya Katiba, na kuhitimiisha ushiriki wa wajumbe wa upinzani (Ukawa), kushiriki kwenye vikao vya Bunge hilo kwa walichodai kuhodhiwa kwa mchakato huo na Chama cha Mapinduzi (CCM), kupitisha Rasimu yao mbadala na kile walichodai kuwa ni kwa wajumbe wa chama hicho kuwatusi na kuwabagua kutokana na sehemu wanazotoka pia wakiwashutumu kwa kueneza chuki makanisani.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akichangia Sura ya Kwanza na ya Pili za Rasimu ya Pili ya Katiba, mjini Dodoma leo jioni.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akichangia Sura ya Kwanza na ya Pili za Rasimu ya Pili ya Katiba, mjini Dodoma leo jioni.
Wajumbe kutoka Vyama vya upinzani pamoja na wale wa taasisi nyingine wanaowaunga mkono wakitoka ukumbini mwa Bunge leo jioni.
Wajumbe kutoka Vyama vya upinzani pamoja na wale wa taasisi nyingine wanaowaunga mkono wakiwa nje ya ukumbi wa Bunge baada ya kutoka leo jioni.
Wajumbe kutoka Vyama vya upinzani pamoja na wale wa taasisi nyingine wanaowaunga mkono wakiwa nje ya ukumbi wa Bunge baada ya kutoka leo jioni.
Wajumbe kutoka Vyama vya upinzani pamoja na wale wa taasisi nyingine wanaowaunga mkono wakiwa nje ya ukumbi wa Bunge wakiondoka kwenda majumbani kwao, baada ya kutoka nje leo jioni.
Wajumbe kutoka Vyama vya upinzani pamoja na wale wa taasisi nyingine wanaowaunga mkono wakiwa nje ya ukumbi wa Bunge wakiondoka kwenda majumbani kwao, baada ya kutoka nje leo jioni.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Wenyeviti wa Vyama vya Chadema, Freeman Mbowe na wa NCCR Mageuzi, James Mbatia wakionesha ishara ya vidole vitatu, ikiwa ndio msimamo wao katika muundo wa Serikali kwa vifungu vya Sura ya Kwanza na ya Sita ya Rasimu ya pili ya Katiba, ambavyo vinajadiliwa na bunge hilo, mjini Dodoma, wakati walipokuwa wakitoka nje ya ukumbi wa Bunge leo, baada ya kile walichokiita kutoridhishwa na hali ya utendaji wa kile walichokiita matusi, kejeli na mipasho kutoka kwa walichodai wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), pamoja na walichodai kampeni zinazofanywa na mmoja wa Mawaziri Makanisani kupinga Serikali tatu zilizopendekezwa na iliyokuwa Tume ya Jaji Joseph Warioba iliyokuwa ikikusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba mpya.
Ukumbi wa Bunge ukionekana kuwa na wajumbe wachache baada ya wajumbe kutoka Vyama vya upinzani na wanaowaunga mkono kutoka taasisi nyingine kutoka nje kutokana na kutoridhishwa kwa kile walichokiita matusi na kejeli za kuwabagua wananchi wa Tanzania.
Hii ndio hali ilivyokuwa ndani ya Bunge baada ya wajumbe kutoka Vyama vya Upinzani na kutoka taasisi nyingine wanaowaunga mkono, kutoka nje ya ukumbi kwa kile walichodai kutoridhishwa na nyendo za wajumbe wa Chama tawala.
Wajumbe kutoka Vyama vya upinzani na wanaowaunga mkono kutoka taasisi nyingine, wakipaza sauti zao baada ya kutoka nje kutokana na kile walichokiita kutoridhishwa na matusi na kejeli za kuwabagua wananchi wa Tanzania kutokana na sehemu wanazotoka. |
No comments:
Post a Comment