TANGAZO


Wednesday, April 16, 2014

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana azindua mradi wa ujenzi wa nyumba 60 Iyonga, Wilaya mpya ya Mlele unaotekelezwa na NHC

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba 60 za makazi ya watu, unaotekelezwa na Shirika la Nyumba ya Taifa (NHC) katika Wilaya ya Mlele mkoani Katavi leo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Shirika la Nyumba Mkoa wa Katavi, Nehemia Msigwa juu ya miradi ya ujenzi wa nyumba itakayofanyika ndani ya mkoa wa Katavi.
Michoro ya nyumba zitakazojengwa mkoani Katavi na Shirika la Nyumba ya Taifa,ambapo wilaya ya Mlele, Shirika la Nyumba linajenga nyumba 60 na zitachukua  miezi nane kukamilika.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dk. Rajab Rutengwe, 
akizungumza mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la uzinduzi wa nyumba 60 zitakazojengwa na Shirika la Nyumba  la Taifa  katika wilaya ya Mlele.
Meneja wa Huduma za Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa Muungano Saguya akizungumzia namna Shirika la Nyumba lilivyojipanga katika kuboresha makazi ya watu katika mkoa wa Katavi. (Picha zote na Adam Mzee (Bashir Nkoromo)

No comments:

Post a Comment