* Wachezaji wa mpira wa miguu wa timu ya Mitaani waliotwaa Ubingwa wa Dunia ndani ya nyumba, Bunge Maalum la Katiba leo
Mwenyekiti wa Kamati namba 1 ya Bunge Maalum la Katiba, Ummy Mwalim, akiwasilisha ripoti ya wengi ya kamati hiyo, katika kikao cha Bunge Maalum la Katiba, mjini Dodoma leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)Mjumbe wa Kamati namba 1 ya Bunge Maalum la Katiba, Eng. Mnyaa, akiwasilisha maoni ya majadiliano ya wachache katika kamati hiyo, kwenye ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd na Waziri wa Sheria na Katiba, Asha Rose Migiro, wakiteta jambo wakati wa uwasilishwaji wa ripoti za kamati 12 za bunge hilo, mjini Dodoma leo.
Mwenyekiti wa Kamati namba 11 ya Bunge Maalum la Katiba, Anna Kilango, akiwasilisha ripoti ya wengi ya kamati hiyo, katika kikao cha Bunge Maalum la Katiba, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Kamati namba 11 ya Bunge Maalum la Katiba, Waziri wa Afya wa Zanzibar, Juma Duni Haji, akiwasilisha maoni ya wachache kwenye kamati hiyo, katika kikao cha bunge hilo kilichokuwa kikipokea ripoti za Kamati 12 za kujadili Sura ya Kwanza na ya 6 ya Rasimu ya Pili ya Katiba, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa bunge hilo, Samuel Sitta (kulia), akimweleza jambo, mjumbe mwenzake, Vita Kawawa Spika wakati wa kikao hicho cha kuwasilisha ripoti za kamati, mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Profesa Mark Mwandosya (kushoto), Vita Kawawa (katikati) na Mohamed Aboud Mohamed (kulia), wakijadiliana jambo, wakati wa uwasilishwaji wa Ripoti za majadiliano yao katika Kamati 12 za bunge hilo, Bungeni mjini Dodoma leo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, wakijadiliana wakati wa uwasilishwaji wa Ripoti za majadiliano yao katika Kamati 12 za bunge hilo, Bungeni mjini Dodoma leo.
Wachezaji wa mitaani walionyakuwa Kombe la Ubingwa wa Dunia, wakiwa na kombe lao hilo ndani ya ukumbi wa Bunge, wakati vijana hao, walipofika bungeni leo kwa mwaliko wa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangala.
Mwenyekiti wa Kamati namba 1 ya Bunge Maalum la Katiba, Ummy Mwalim, akishangiliwa na kupongezwa na baadhi ya wajumbe waliofurahishwa na uwasilishaji wa ripoti ya wengi ya kamati hiyo, katika kikao cha Bunge Maalum la Katiba, mjini Dodoma leo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (katikati), akiwa na katika picha ya pamoja na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangala pamoja na wachezaji wa mitaani walionyakuwa Kombe la Ubingwa wa Dunia, wakati vijana hao, walipofika bungeni leo kwa mwaliko wa waziri huyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, akisalimiana na Kapteni msaidizi, Frank William wa timu ya Vijana wa mitaani, iliyonyakua Kombe la Ubingwa wa Dunia wakati walipofika bungeni leo kwa mwaliko wa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangala, mjini Dodoma.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akikabidhiwa Kombe la Ubingwa wa Dunia na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangala, lililonyakuliwa na watoto wa mitaani wakati vijana hao, walipofika bungeni leo kwa mwaliko wa waziri huyo.
Mjumbe wa Kamati namba 11 ya Bunge Maalum la Katiba, Waziri wa Afya wa Zanzibar, Juma Duni Haji (katikati), akisindikizwa kwa shangwe na baadhi ya wajumbe baada ya kufurahishwa na jinsi alivyowasilisha maoni ya wachache kwenye kamati hiyo, katika kikao hicho leo.
No comments:
Post a Comment