Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.
HIRIKISHO la ngimi Tanzania (BFT) linatoa pongezi za dhati kwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Mh. Bernard Membe kwa
hatua na jitihada alizozifanya za
kutafua na kufanikisha kambi ya mazoezi
kwa Timu ya Taifa ya ngumi inayojiandaa
kushiriki mashindano ya jumuiya ya madola yatakayofanyika July, 2014 Nchini
Scotland.
Kwa
hakika ni mmoja wa watanzania ambae ameguswa na maandalizi ya Timu yetu ya Taifa kwa kuitafatia kambi ya mazoezi ya kimataifa Nchini Uturuki
na Nchini China kwani timu yetu ilikuwa inafanya mazoezi katika hali duni bila ya kuwa na vifaa vya kisasa kulingana na
mabadiliko ya mchezo wa ngumi duniani.
Kwa
kufanya hivyo tunakuwa na uhakika mkubwa wa kupata medali katika mashindano
hayo ya Jumuiya ya Madola na Tanzania kutangazika vema Kimataifa kupitia mchezo
wa ngumi maana bado tunakumbuka historia nzuri ya ushiriki waTanzania katika
mashindano ya Jumuiya ya madola kwani kwa mara ya kwanza Tanzania ilishiriki
mwaka 1972 na Tanzania kupata medali ya
kwanza ya kimataifa baada ya Tanzania
kupata uhuru, iliyoletwa na Bondia (LYTUS
SIMBA) na baada ya hapo baadhi ya mabondia walioleta medali ni kama wafuatao:
MICHAEL YOMBAYOMBA
: (Dhahabu)
HAJI MATUMLA : (Fedha)
MAKOYE ISANGURA : (Shaba )
MWAMBEYA
BAKARI : (Shaba )
WILLY
ISSANGURA : (Shaba )
LUCAS MSOMBA : (Shaba )
Bado BFT tunamuomba azidi kutusaidia vifaa zaidi hasa ulingo wa kisasa na Computer
inayotumika kuhesabia point za ushindi
wakati wa mashindano kwani Nchi zote duniani ndizo wanazozitumia na niagizo
kutoka chama cha ngumi cha dunia kwa wanachama wote lazima waitumie katika
mashindano..
Taarifa hii imeletwa kwenu na
Makore Mashaga
KATIBU MKUU.
No comments:
Post a Comment