Mkuu wa shirika la Umoja wa
Mataifa la haki za binadamu , Navi Pillay yuko nchini Sudan kusini
kutathmin hali huko baada ya miezi minne ya mzozo .
Ziara yake inakuja siku kadhaa tu baada ya watu
wenye silaha kushambulia kambi ya Umoja wa Mataifa iliyoko Bor, na
kuwauwa takriban watu 58 wakiwemo wahudumu na watoto .Bi Pillay atakutana pia na watu walioyahama makazi yao kutokana na vita. Juma lililopita mamia ya raia waliuawa Bentiu-- mji mkuu wa jimbo lenye utajiri wa Mafuta .
Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Kusini , Barnaba Mariel Benjamin ameiambia BBC kuwa serikali yake inataraji Umoja wa Mataifa utalaani mauaji ya raia wanayolaumiwa kuyafanya waasi .
Wakati huo huo wawakilishi wa pande husika na mzozo huo wamerejea mjini Addis Ababa Ethiopia kufufua mazungumzo ya amani
No comments:
Post a Comment