Ajali ya helikopta nchini
Afghanistan ambayo imeua askari wote watano wa Uingereza waliokuwa ndani
ya helikopta hiyo ni "ajali ya kusikitisha", Wizara ya Ulinzi ya
Uingereza imesema.
Helikopta hiyo, aina ya Lynx ilianguka chini kusini mwa Afghanistan, Jumamosi.Waziri Mkuu David Cameron ametoa rambirambi kwa askari hao, ambao familia zao zimekwishaarifiwa kuhusu mkasa huo.
Askari watatu kati yao na mwanaanga mmoja wanatoka kambi ya kijeshi ya Hampshire. Askari wa tano, ambaye alikuwa katika kikosi cha jeshi la akiba, anatoka jijini London.
Hii ni ajali ya kwanza mbaya kusababisha vifo vya askari wote ikihusisha helikopta ya kijeshi ya Uingereza katika mgogoro wa Afghanistan lakini ni tukio la tatu kubwa kabisa kwa askari wa Uingereza kupoteza maisha katika tukio moja la ajali nchini Afghanistan tangu nchi hiyo ivamiwe na majeshi ya washirika mwaka 2001.
No comments:
Post a Comment