Mkurugenzi Muwezeshaji wa Mfuko wa Jamii Zanzibar (ZSSF), Abdulwakil Haji Hafidh, akizungumza na Wajasiriamali Wanawake wanaofanya biashara katika viwanja vya Michezani, Kisonge (Sunday Market), wakati wa hafla ya kuwakabidhi mashamiana mawili kwa ajili ya kuweka wakati wakiwa katika eneo hilo, kwa ajili ya kujikinga na jua ili waweze kufanya biashara zao kwa uhakika baada ya kukosa huduma hiyo kwa muda mrefu na kulazimika kukaa chini ya miti kufanya biashara zao hizo. (Picha zote kwa hisani ya Zanzinews Blog)
Wajasiriamali wa vikundi vya wanawake, wakimsikiliza Mkurugenzi Mwendeshaji wa mfuko wa ZSSF Zanzibar, wakati akitoa nasaha zake katika hafla ya kuwakabidhi mashamiana ya kujikinga na jua na mvua.
Maofisa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) wakifuatilia hafla hiyo, iliofanyika katika Viwanja vya Michezani, Kisonge, mjini Unguja leo.
Mwakilishi wa Wajasiriamali Sundy Market Michezani, Bi. Fatma Hamran akitowa shukrani kwa niaba ya wanachama wa vikundi vya Wajasiriamali wanawake kwa msaada huo, waliopokea kutoka kwa ZSSF, na kusema kuwa umefika wakati muafaka na hasa katika kipindi hichi cha mvua za Masika zinazotarajiwa kuaza wakati wowote kuazia sasa, "mashamiana haya yatatusaidia katika kipindi hicho na kipindi cha jua, takriba sasa tuko chini ya mti tukifanya biashara zetu", alisema.
Ofisa Uhusiano wa ZSSF, Mussa Yussuf akitoa maekelezo baada ya kumalizika kwa kukabidhi mashamiana hayo kwa Wanawake Wajasiriamali wa Sunday Markert, Michezani Kisonge.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZSSF, Abdulwakil Haji Hafidh, akitembelea na kuona bidhaa mbalimbali za Wajasiriamali kwenye mabada yao.
No comments:
Post a Comment