TANGAZO

Sunday, March 30, 2014

Waziri Kabaka afungua michuano ya NSSF Cup

*Jambo Leo Netiboli yatoa kipigo kwa Habari, Maelezo
*Yaitandika mabao 60-8
* Nayo Habari Zanzibar yaitandika New Habari mabao 4-1, mpira wa miguu

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo. Wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Chiku Matesa.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Chiku Matesa (kulia), akibadilishana mawazo na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka wakati wa uzinduzi wa michuano hiyo.

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akisalimiana na mshambuliaji wa timu ya New Habar 2006, Joh Dande wakati wa uzinduzi wa michuano ya NSSF Media Cup 2014 kwenye uwanja wa TCC Chang'ombe Dar es Salaam leo.
Mchezaji wa New Habari, Jonathan Tito, akimiliki mpira huku akizongwa na mshambuliaji wa timu ya Habari Zanzibar, Hamza Hamza katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya NSSF Media Cup uliofanyika kwenye Uwanja wa TTC, Chang’ombe jijini Dar es Salaam leo. Habari Zanzibar ilishinda 4-1. (Na Mpiga Picha Wetu)
Mchezaji wa timu ya netiboli ya Jambo Leo (kushoto), akimiliki mpira wakati timu hiyo ilipopambana Habari-Maelezo. Jambo leo ilishinda  ilishinda 60-8.
Mchezaji wa timu ya netiboli ya Jambo Leo (kushoto), akimiliki mpira wakati timu hiyo ilipopambana Habari-Maelezo. Jambo leo ilishinda  ilishinda 60-8.
Kikosi cha mpira wa Netiboli cha Jambo Leo, kilichotoa kipigo kwa timu ya Habari-Maelezo leo.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, akirusha mpira kwenye pete kufungua mashindano ya NSSF Media Cup, kwa upande wa mpira wa Netibali kwenye Viwanja vya Sigara (TCC), Chang'ombe jijini Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment