Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akizungumza na wanawake mbalimbali (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa Bonanza la Mpira wa Kikapu lililoandandiliwa na Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) leo jijini Dar es Salaam katika viwanja vya DUCE. Kushoto ni Mkuu wa Kitivo cha Sayansi chuoni hapo Dkt. Constansia Rugumamu na kuli ni Kamishina wa wanawake TBF Bi. Angella Grolia Bondo. (Picha zote na Frank Shija - WHVUM)
Kamishina wa wanawake TBF Bi. Angella Grolia Bondo akitoa maelezo kuhusu Bonanza la Mpira wa Kikapu waliloandaa kwa ajili ya kuadhimisha siku ya wanawake dunia, Mwenye koti jeupe ni jijini Dar es Salaam katika viwanja vya DUCE. Kushoto ni Mkuu wa Kitivo cha Sayansi chuoni hapo Dkt. Constansia Rugumamu na kulia ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika bonanza hilo.
Spika wa Bunge la wanafunzi wa DUCE Bi. Hawa Magoti akielezea jambo wakati wa ufunguzi wa Bonanza la Mpira wa Kikapu lililoandandiliwa na Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) leo jijini Dar es Salaam katika viwanja vya DUCE kutoka kushoto ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika bonanza hilo, katikati ni Mkuu wa Kitivo cha Sayansi chuoni hapo Dkt. Constansia Rugumamu.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara (kushoto), akifurahia zawadi ya picha yake ambayo imetolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Bw. Dioniz Malinzi (hayupo pichani) na kukabidhiwa kwa niaba yake na Kamishna wa wanawake TBF Bi. Angella Grolia Bondo leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akifurahia zawadi yake na baadhi ya wanafunzi wa kike waliosuka nywele kwa mtindo kama wake.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akielekea uwanjani tayari kwa kuzindua rasmi bonanza hilo.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara, akisikiliza kwa makini maelezo kuhusu huduma za NSSF (ambao ndiyo wadhamini wa bonanza hilo) kutoka kwa Ofisa Uhusiano wa shirika hilo Bi. Maife Kapinga mara baada ya kuwasili uwanjani tayari kwa kufungua bonanza leo jijini Dar es Salaam. NSSF ndiyo wadhamini wakuu wa bonanza hilo.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akikagua wachezaji wa timu ya Don Bosco Lioness kabla ya mchezo wao kuanza. Mechi ya ufunguzi wa bonanza ilikuwa kati ya Jeshi Star na Don Bosco Lioness ambapo hadi mchezo unamalizika Don Bosco Lioness waliibuka kidedea kwa jumla ya Vikapu 23 dhidi ya 19 vya Jeshi Star.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiongea na wachezaji kabla ya mchezo kuanza.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akirusha mpira kwenye pete, kuashiria ufunguzi rasmi wa bonanza hilo
Mchezaji wa timu ya Don Bosco Lioness akipiga shot baada ya kutendewa madhambi.
No comments:
Post a Comment