TANGAZO


Saturday, March 8, 2014

Wanamgambo wa Libya wasafirisha mafuta


Bandari moja ya mafuta ya LIbya
Kundi la wanamgambo waliovamia bandari za Libya zinazosafirisha mafuta, limeiambia BBC kwamba limeanza kusafirisha mafuta na shehena ya kwanza ilipakiwa kwenye meli yenye bendera ya Korea Kaskazini.
Waziri mdogo wa mafuta amethibitisha kuwa meli hiyo imefunga gati katika bandari ya Sidr ambayo inadhibitiwa na kundi linalotaka kujitenga.
Serikali ya Libya inashindwa kuanza tena kusafirisha mafuta hadi nchi za nje kwa sababu ya migomo katika bandari na visima vya mafuta kutekwa na wanamgambo.
Serikali inahitaji pato linalotokana na mafuta ili kuendesha uchumi wa nchi.

No comments:

Post a Comment