TANGAZO


Saturday, March 1, 2014

Obama aionya Urusi kuhusu Ukraine





Rais Barack Obama wa Marekani

Rais Barack Obama wa Marekani ameionya Urusi, kuwa hatua yoyote ya kuingilia kijeshi mgogoro wa Ukraine itakuwa na madhara makubwa.
Bwana Obama amesema amesikitishwa na taarifa za kuwepo harakati za majeshi ya Urusi nchini Ukraine.
Kaimu rais wa Ukraine,Olexander Turchynov, ameishutumu Urusi kwa kupeleka vikosi vyake katika jimbo la Crimea nchini Ukraine ili kutaka kuibua "mgogoro wa kijeshi".
Waziri mkuu wa Crimea anayeipendelea Urusi, ameiomba serikali ya Urusi kusaidia kuimarisha amani katika jimbo hilo.
"Namwomba rais wa Shirikisho la Urusi, Vladimir Putin, kutoa msaada ili kuimarisha amani na utulivu katika jimbo la Crimea lenye mamlaka ya kuijiamulia mambo yake lenyewe." Amesema Bwana Serhiy Aksyonov katika taarifa.
Bwana Aksyonov, ambaye aliteuliwa na bunge la Crimea siku ya Alhamisi, pia amesema anashikilia kwa muda wizara ya mambo ya ndani ya Crimea, majeshi, usafiri na ulinzi wa mipaka.
Tangu kuondolewa madarakani kwa Rais Victor Yanukovych wa Ukraine ambaye kwa sasa yuko uhamishoni nchini Urusi, mgogoro umehamia katika jimbo la Crimea, ambalo wakaazi wake ni Warusi.

No comments:

Post a Comment