TANGAZO


Tuesday, March 25, 2014

Nape Nnauye anogesha kampeni za Ridhiwani Kikwete Chalinze

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye akiandamana na wananchi kwenda kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi wa mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze, kupitia chama hicho, Ridhiwan Kikwete katika Kijiji cha Mkoko, Kata ya Msata, wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani leo.
Akina dada, wafuasi wa CCM wakiwa na mabango yenye picha ya mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kupitia chama hicho, Ridhiwani Kikwete, wakielekea kwenye mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Mkoko, Kata ya Msata Wilayani Bagamoyo, ambapo Mratibu wa kampeni hizo Kitaifa, Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alihutubia na alimuombea kura mgombea huyo.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damiani Lubuva (kushoto), akisalimiana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (wa pili kulia) na Kaibu wa CCM Mkoa wa Mtwara, Shaibu Akwilombe ambapo yeye na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Julius Malaba, walikuwepo kuangalia kampeni za CCM katika Kijiji cha Madesa, Kata ya Msata, wilayani Bagamoyo, mkoa wa Pwani.
Nape Nnauye, akihutubia wakati wa mkutano wa kumnadi Ridhiwani Kikwete katika Kijiji cha Pongwe Msungula, Kata ya Msata.
Wafuasi wa CCM, wakishangilia wakati wa mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Kihangaiko, Kata ya Msata.
Nape akihutubia katika Kijiji cha Kihangaiko, wakati wa mkutano huo. (Picha zote kwa hisani ya Kamanda wa Matukio Blog)

No comments:

Post a Comment