Rais Robert Mugabe ameamua kupunguza hasira ya umma kwa kukata mishahara ya wakuu wa makampuni yanayo milikiwa na serikali.
Mugabe mwenye umri wa miaka 90 amekuwa akikabiiliwa na shinikizo kubwa kuchukua hatua baada ya kufichuliwa kwa taarifa kwamba wengi wa vigogo hao wanapokea kitita cha hadi dola $500,000 kwa mwezi.
Kipato cha wastani cha mhudumu wa serikali nchini Zimbabwe ni dola $370 kwa mwezi.Serikali yake itapunguza malipo ya wakuu wa taasisi hadi dola 72,000 kwa mwaka, yakiwemo marupurupu .
" Mbele ya macho ya umma , mishahara hii minono na marupurupu si ufisadi tu bali ni aibu ," Alieleza waziri wa fedha Patrick Chinamasa .
Ilifichuliwa kuwa mkuu wa shirika la habari la taifa la Zimbabwe (ZBC) alikuwa akipokea kitita cha dola 37,050 pesa taslim kila mwezi , ili hali chombo hicho cha habari kinachodhibitiwa na serikali kilishindwa kuwalipa wafanyakazi wake kwa zaidi ya miezisita mwaka jana.
Sakata nyingine iliyojitokeza ni kwamba - moja ya kampuni ya bimma ya matibabu kwa waajiriwa ilikuwa ikimlipa mkurugenzi wake mkuu mshahara kiasi cha dola 230,000 huku kila mwezi ikimpatia marupurupu ya dola $305,499 ya malipo hayo.
Mwandishi wa BBC aliyeko mjini Harare Brian Hungwe , anasema kashfa hiyo iliyobandikwa jina "salarygate", iliibuka mwishoni mwa mwaka jana.
No comments:
Post a Comment