TANGAZO


Monday, March 24, 2014

Marekani kusaidia UG kupambana na Kony



Kiongozi wa waasi wa LRA Joseph Kony
Serikali ya Marekani inatuma ndege za kivita na kikosii maalum cha jeshi kusaidia Uganda katika juhudi za kumsaka kiongozi wa kundi la waasi la Lord's Resistance Army, Joseph Kony.
Msemaji wa baraza la usalama la Marekani, Caitlin Hayden, amesema kuwa wanajeshi wa Afrika wataendelea kuongoza operesheni hiyo, ingawa watapata ushauri kutoka kwa vikosi vya Marekani.
Alisema kuwa ndege hizo zitawekwa nchini Uganda ingawa zitatumika katika nchi zingine ambako waasi wa LRA wamekuwa wakijificha.
Marekani ilituma vikosi vyake mara ya kwanza nchini Uganda mwaka 2011 kusaidia Uganda katika harakati za kumtafuta Joseph Kony.

No comments:

Post a Comment