Watafiti kutoka Uingereza na
Marekani wanasema kuwa mabadiliko ya hali ya hewa huenda yakazua
ongezeko kubwa la maambukizi ya ugonjwa wa Malaria kote duniani huku
ugonjwa huo ukienea katika maeneo ya milimani barani Afrika na Amerika
ya Kusini.
Katika matokeo ya utafiti yaliyochapishwa kwenye
jarida la Science, wanasayansi hao wanasema hata ongezeko dogo katika
viwango vya joto siku za usoni huenda likaongeza kwa mamilioni
maambukizi ya malaria.Watu wanaoishi katika maeneo ya nyanda za juu wanakosa kinga na hivyo kurahisisha maradhi ya malaria kuenea.
Takriban watu milioni mia mbili ishirini kote duniani huambukizwa ukonjwa wa malaria.
No comments:
Post a Comment