Maafisa wawili wa jeshi nchini Misri pamoja na wapiganaji watano wa kiisilamu, wameuawa katika makabiliano ya risasi, wakati jeshi lilipokuwa linafanya msako Kaskazini mwa Cairo.
Maafisa hao wa vyeo vya Brigadia na Kanali na wenye ujuzi wa kutegua mabomu, walihusika katika msako huo walioufanya katika ghala la silaha katika mkoa wa Qalyubia wakishirikiana na vikosi maalum.
Maafisa walisema kuwa wapiganaji hao ni wa kundi la wapiganaji la Ansar Beit al-Maqdis, ambalo wamekiri kufanya mashambulizi kadhaa.Mabomu yaliteguliwa wakati wa makabiliano hayo ambayo yalidumu kwa saa kadhaa.
Kundi hilo linalohusishwa na al-Qaeda na ambalo lina makao yake katika rasi ya Sinai, linaaminika kuwaua zaidi ya maafisa 200 wa usalama pamoja na maafisa wnegine wa serikali tangu jeshi kumwondoa mamlakani aliyekuwa Rais Mohammed Morsi mwezi Julai.
Msako huo uliofanywa Julai, ulitokana na uchunguzi ulioonyesha ghala hiyo ya silaha ikitumiwa kama kiwanda cha kutengeza mabomu.
No comments:
Post a Comment