Wajumbe kutoka mataifa 25,ya Afrika pamoja na wadau wa sera za uongozi bora kutoka sehemu mbali mbali duniani wanaanza mkutano wao mjini Kigali,utakaodumu siku tano,kuhusiana na mikakati ya uongozi bora kama nyenzo za maendeleo endelevu.
Mkutano huo umeandaliwa kwa ushirikiano wa serikali ya Rwanda na shirika linalohimiza sera za uongozi bora duniani la Ujerumani GTZ.
''Governance and Decentralization"yaani jinsi uongozi unavyopaswa kuwajibikiwa kwa kuhakikisha maendeleo ya wananchi na kupeleka karibu mamlaka ya kiutawala kwa wananchi ndiuo kauli mbiu ya mkutano huo.Mada pekee inahusu "International Symposium on Accountable'
Rwanda ni moja ya mataifa yanayotajwa kufanya vyema katika sera za kupeleka karibu na wananchi mamlaka ya kiutawala na mikakati imara ya uongozi bora hasa katika vita dhidi ya rushwa.
Hata hivyo inatajwa kukabiliwa na changamoto kadhaa za ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma miongoni mwa baadhi ya viongozi ambapo viongozi kadhaa wanaandamwa na tuhuma za ubadhilifu wa mali ya umma kupitia ripoti ya mkaguzi mkuu mali ya umma.
Washiriki wa kongamano hilo wanataraji kutembelea jamii ya wanyarwanda vijijini na kushuhudia mazingira ya utawala wa kimikoa.
Rwanda inaadhimisha muongo mmoja wa utekelezaji wa sera za kupeleka mamlaka karibu na wananchi.Sera hiyo nchini Rwanda, ilianza mnamo mwaka 2000.
Suala la Uongozi mbaya linaripotiwa kuwa chanzo cha migogoro katika mataifa duniani na hasa pale panapotokea sehemu ya jamii kujilimbikizia keki ya taifa na kusahau sehemu nyingine ya jamii.
Hii imejitokeza katika mifano mbali mbali ya mataifa ya Afrika.
No comments:
Post a Comment