Waziri Said Ali Mbarouk |
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mh. Said Ali
Mbarouk anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la muziki wa kizazi kipya
na tenzi, linalotajiwa kufanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers jijini
Dar es salaam kesho.
Tamasha hilo ni maalum
kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 50 ya
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar . Kauli mbiu za maadhimisho ya mwaka huu ni Utanzania
wetu ni Muungano wetu tuulinde , tuuimarishe na kuudumisha.
Tamasha hilo ni sehemu ya
shughuli mbalimbali zinazotarajiwa kufanyika kuelekea kilele cha Miaka 50 ya Muungano
tarehe 26.4.2014.
Maadhimisho ya miaka 50
ya Muungano yataambatana na shughuli mbalimbali zitakazowashirikisha wananchi
kupitia makangomano, michezo na burudani na kilele chake itakua tarehe 26
Aprili,2014.
Shughuli zitakazofanyika ni pamoja na
kongamano na utengamano wa kikanda wa Afrika Mashariki, kongamano la Bara la
Afrika ,tamasha la muziki wa dansi na taarabu , maonyesho ya Idara na Wizara za
Muungano na mkesha utakaofanyika kuamkia
siku ya Muungano.
Aidha maadhimisho haya ya
miaka 50 ya Muungano yalizinduliwa Machi 1, 2014 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein kwenye ukumbi wa Salama katika hoteli ya
Bwawani Mjini Unguja msisitizo ukiwekwa kwa wananchi kuendelea
kudumisha udugu, amani, umoja na mshikamano.
No comments:
Post a Comment