Charles Ble Goude, mshirika mkubwa wa Rais wa zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo, amefikishwa kwa mara ya kwanza katika mahakama ya kimataifa ya jinai ICC.
Bwana Ble Goude, aliyekuwa waziri wakati mmoja, anatuhumiwa kwa kutenda uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu nchini Ivory Coast mwaka 2010.
Hatua ya kumkabidhi Charles Ble Goude kwa mahakama ya ICC, iliwakasirisha sana wafuasi wa Gbagbo, ambaye yuko katika mahakama hiyo ya Hague akisubiri kuanza kusikilizwa kwa kesi yake.Amekanusha madai hayo ikiwemo kuongoza kikundi cha wapiganaji.
Kibali cha kukamatwa kwa Ble Goude kilitolewa mwezi Septemba.
Wendesha mashitaka katika mahakama ya ICC, wanamtuhumu Ble Goude kwa kuongoza, ghasia hizo , tuhuma za ubakaji, mauaji na kuwatesa watu.
Uhalifu huo ulitendwa kati ya Disemba mwaka 2010 hadi Aprili 2011 baada ya mgogoro kuibuka kuhusu mshindi wa uchaguzi mkuu.
Takriban watu 3,000, walipotza maisha yao baada ya bwana Gbagbo kukataa kukubali kushindwa kwenye uchaguzi huo dhidi ya mpinzani wake Alassane Ouattara.
Ble Goude alikuwa kiongozi wa tawi la vijana wazalendo wa chama tawala, ambao walilaumiwa kwa kufanya ghasia na kusababisha vifo nchini humo.
No comments:
Post a Comment