*Kikao chaingia mtafaruku
*Wajumbe waanza kutupiana maneno ya kejeli
*Mwenyekiti wa Muda alazimika kukiaighirisha
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri wa Sheria wa Serikali ya Zanzibar, Aboubakar Khamis Bakari (kushoto), akizungumza ndani ya ukumbi wa Bunge baada ya kudai kuchafuliwa na mjumbe mwenzake wa bunge hilo, Ole Sendeka, hatua iliyosababisha kuzuka vurugu katika kikao cha bunge hilo, mjini Dodoma leo asubuhi. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Wajumbe wa Bunge hilo, wakizozana katika mtafaruku uliotokea bungeni humo leo asubuhi, wakati wa kuchangia Rasimu ya Kanuni za bunge hilo, mjini Dodoma.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, wakinyanyuka kwenye viti na kisha kuondoka baada ya Mwenyekiti wa muda, Pandu Ameir Kificho kuaghirisha kikao cha bunge hilo baada ya kuzuka mtafaruku huo.
Hali ya ndani ya ukumbi wa Bunge, ilivyokuwa wakati wa vurugu hizo.
Wajumbe wa bunge hilo, wakinyanyuka kwenye viti vyao baada ya Mwenyekiti wa muda, Pandu Ameir Kificho kuaghirisha kikao cha bunge hilo baada ya kuzuka mtafaruku huo.
Wajumbe wa bunge hilo, wakinyanyuka kwenye viti vyao baada ya Mwenyekiti wa muda, Pandu Ameir Kificho kuaghirisha kikao cha bunge hilo baada ya kuzuka mtafaruku huo.
Wajumbe wa Bunge hilo, wakitoka nje ya ukumbi baada ya kuaghirishwa kikao hicho kutokana na kuzuka kwa mtafaruku wa kutokuelewana.
Wajumbe wa bunge hilo, wakiwa nje ya ukumbi wa Bunge, wakielezana kuhusu kilichotokea mpaka kuzuka kwa mtafaruku huo.
Wajumbe wa Bunge hilo, wakitoka nje ya ukumbi baada ya kuaghirishwa kikao hicho kutokana na kuzuka kwa mtafaruku wa kutokuelewana.
Wajumbe wa bunge hilo, wakiwa nje ya ukumbi wa Bunge, wakijadili kuhusu kilichotokea mpaka kuzuka kwa mtafaruku huo.
Wajumbe wa bunge hilo, wakiwa wamekaa kundi nje ya ukumbi wa Bunge, wakielezana kuhusu kilichosababisha kuzuka kwa mtafaruku huo.
Wajumbe wa bunge hilo, wakiwa wamekaa kundi nje ya ukumbi wa Bunge, wakielezana kuhusu kilichosababisha kuzuka kwa mtafaruku huo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa (kushoto), akizungumza jambo na mjumbe mwenzake, Saleh Pamba, nje ya Bunge, baada ya kuzuka kwa mtafaruku huo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mansoor Hiran, akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Bunge, mara baada ya kuzuka kwa vurugu hizo na kuaghirishwa kwa kikao cha kujadili Rasimu ya Kanuni za bunge hilo, mjini Dodoma leo asubuhi.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freema Mbowe, akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Bunge, kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo kuzuka kwa vurugu hizo, katika kikao cha kujadili Rasimu ya Kanuni za bunge hilo, mjini Dodoma leo asubuhi.
No comments:
Post a Comment