* Afurahishwa na upanuzi wa mitambo ya maji ya Ruvu chini
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, akiwaongoza viongozi wa chama hicho Wilaya ya Kinondoni, kutembelea mitambo mipya baada ya upanuzi wa mitambo ya maji ya Ruvu Chini, wilayani Bagamoyo, kufanyika. Ujenzi wa mitambo hiyo, umegharimu sh. Trilioni 1.6. Mradi huo unaotarajia kukamilika mwaka huu utapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la maji katika Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida.
Kinana (wa pili kulia), akipata maelekezo kutoka kwa Ofisa wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka, kuhusu mitambo mipya ya maji ya Ruvu chini alipotembelea leo.
Kaibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwaongoza viongozi wa CCM Wilaya ya Kinondoni kutembelea mitambo mipya baada ya upanuzi wa mitambo ya maji ya Ruvu Chini, wilayani Bagamoyo, kufanyika. Ujenzi wa mitambo hiyo, umegharimu sh. Trilioni 1.6. Mradi huo, unaotarajia kukamilika mwaka huu, utapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la maji katika Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida.
Kinana akiangalia sehemu ya mitambo mipya ya maji ya Ruvu Chini.
Kinana akipata maelezo kutoka kwa Ofisa wa Dawasa kuhusu mitambo hiyo mipya.
Kinana akizungumza na vyombo vya habari kuhusu jinsi alivyofurahishwa na ujenzi wa mitambo hiyo ya maji.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadicky
Kinana akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida.
Kinana akitoka kuangalia mitambo mipya ya kusukuma maji kutoka Ruvu Chini kwenda Mikoa wa Pwani na Dar es Salaam.
Kinana akiangalia sehemu ya kuchanganyia dawa za maji kabla ya kusafirishwa kwa matumizi.
Matrekta yakiendelea na kazi ya ukamishaji wa ujenzi wa mitambo hiyo.
Kinana akikata kiu kwa kunywa maji ya dafu nje kidogo ya Mji wa Bagamoyo, baada ya kutoka kutembelea mitambo mipya ya Maji ya Ruvu Chini leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki, akikata kiu kwa kunywa maji ya dafu, nje kidogo ya Mji wa Bagamoyo, baada ya kutoka kutembelea mitambo mipya ya Maji ya Ruvu Chini leo.
Kinana akihutubia wafuasi wa CCM wa Bajaji na Bodaboda eneo la Darajani Kawe, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Kinana akiwa na Meya wa Kinondoni, Mwenda wakitembelea Kituo kipya cha Polisi, kilichojengwa kwenye kituo kipya cha daladala eneo la Ubungo leo.
Sehemu ya vibanda vya abiria vilivyojengwa katika kituo hicho.(Picha zote kwa hisani ya Kamanda wa Matukio Blog)
No comments:
Post a Comment