TANGAZO


Friday, March 28, 2014

Kampuni kubwa za Ujenzi kutoka Uturuki zavutiwa na Tanzania

Mtendaji Mkuu wa ampuni ya KAYA Bw. Orhan Babaoglu (kushoto) akiwasilisha kwa Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, utambulisho wa makampuni ya Uturuki ambayo yamefungua Ofisi hapa nchini kwa lengo la kushiriki katika kazi za kandarasi za ujenzi hapa nchini.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipitia baadhi ya nyaraka zilizowasilishwa na makampuni ya kandarasi kutoka Uturuki. Wengine katika picha (kutoka kulia) ni Naibu Katibu Mkuu Eng. Joseph Nyamhanga, Katibu Mkuu Alhaj Mussa Iyombe na kushoto kabisa ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya KAYA Bw. Orhan Babaoglu.
Bw. Kursat Durak (aliyenyoosha mkoni), kutoka Kampuni ya CEYTUN ya Uturuki akifafanua jambo. Wengine katika picha (kutoka kulia) ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya KAYA Bw. Orhan Babaoglu, Bw. Hassan Tunk Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya CEYTUN na kushoto kabisa ni Bw Remzi Demircan Mbia wa Kampuni ya KAYA.

Na Martin Ntemo
KAMPUNI kadhaa kutoka nchi ya Uturuki zimeanza kuingia Tanzania ili kushiriki katika kazi za ujenzi kwenye maeneo mbali mbali hapa nchini. Kukua kwa sekta ya ujenzi kumekua ndiyo kivutio kikuu kilichozifanya kampuni hizo, kuonyesha nia ya kufungua ofisi zao hapa nchini.

Wakizungumzi katika kikao na Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli walipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam, wawakilishi kutoka Kampuni Kampuni tatu tofauti wamempongeza waziri huyo kwa jinsi anavyosimamia sekta hiyo ya ujenzi kiasi cha kuanza kuvutia makampuni makubwa kutoka nje.

“Tumekuwa tukifuatilia uendeshwaji na ukuaji wa sekta ya ujenzi katika mataifa kadhaa barani Afrika na tumejiridhisha kuwa Tanzania ni nchi inayofanya vizuri katika upande huo” alibainisha Bw. Orhan Babaoglu ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya KAYA ya Uturuki.

Mwakilishi mwingine kutoka Kampuni ya CEYTUN ya huko huko Uturuki Bw. Kursat Durak amebainisha kuwa, utendaji wa kampuni za Kituruki unafahamika duniani kote, hivyo ujio wao unalengo la kuamsha ushidani wa ubora lakini pia kuona kuwa gharama za utekelezaji wa miradi hiyo zinathibitiwa kwa kuwa na washindani kutoka maeneo tofauti.

Mhe. Magufuli kwa upande wake wakati akiwakaribisha amewataka kuzingatia sheria na taratibu zinaoongoza shughuli za kandarasi hapa nchini. Waziri Magufuli aliwajulisha kuwa, mbali na kazi za kawaida za kandarasi kwa hivi sasa kuna miradi kadhaa mikubwa inayokusudiwa kuendeshwa kwa kushirikisha sekta binafsi hivyo hiyo pia ni fursa wanayoweza kujishughulisha nayo hapa nchni.  

No comments:

Post a Comment