TANGAZO


Thursday, March 6, 2014

Kampeni za CCM Jimbo la Kalenga zatikisa Kata ya Ifunda


Wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakishangilia kwa furaha baada ya kufurahishwa na hotuba ya mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga, kupitia chama hicho, Godfrey Mgimwa katika Kijiji cha Kibena, Kata ya Ifunda, Iringa vijijini leo.
 Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi, Miraji Mtaturu (kulia), akimnadi kwa wananchi mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, katika Kijiji cha Mibikimtali, Kata ya Ifunda, Iringa Vijijini leo.
Wafuasi wa CCM, wakishangilia baada ya kufurahishwa na hotuba ya mgombea wa chama hicho, Godfrey Mgimwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kijiji cha Mibikimitali, Kata ya Ifunda leo.
Akina mama wakishangilia na kupiga makofi baada ya kufurahishwa na hotuba ya mgombea wa CCM, Godfrey Mgimwa.
Mgimwa akihutubia katika mkutano wa kampeni katika Kijiji cha Mibikimitali, Kata ya Ifunda leo.
 Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Mko wa Arusha, Rehema Mohamed akimuombea kura mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kuptia CCM, Godfrey Mgimwa katika mkutano wa kampeni kwenye Kijiji cha Kibena, Kata ya Ifunda, Iringa Vijijini leo.
 Wafuasi wa CCM wakisikiliza kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kupitia CCM, Godfrey Mgimwa katika Kijiji cha Kibena, Kata ya Ifunda, Iringa Vijijini leo.
Wafanyabiashara wa mbogamboga, wakisikiliza kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na mgombea wa CCM, Godfrey Mgimwa.
 Ofisa wa Umoja wa Vijana wa CCM, Makao Makuu, Mwampamba akimnadi kwa wananchi mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa.
 Wananchi wakifurahi na kupiga makofi, wakati wakisikiliza hotuba ya mgombea wa CCM, Godfrey Mgimwa katika Kijiji cha Kibena leo.
 Meneja a Kampeni za CCM katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga, Meja mstaafu Mbuta akielezea kwa wananchi sababu za kumpigia kura Mgimwa wa CCM, badala ya mgombea wa Chadema. Grace Tendega
Katibu wa CCM, Wilaya ya Mufindi, Miraji Mtaturu akimfayia kampeni Mgimwa katika Kijiji cha Kibena leo. (Picha zote kwa hisani ya Richard Mwaikenda wa Kamanda wa Matukio blog)

No comments:

Post a Comment