TANGAZO

Tuesday, March 18, 2014

Jaji Warioba awasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba katika Bunge la Katiba mjini Dodoma leo

* Rasimu yapendekeza Mawaziri wasitokane na wabunge
*Kusiwe na chaguzi ndogo za wabunge wanapofariki

Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Steven Wasira na Anjela Kairuki, wakisalimiana wakati wakielekea kwenye ukumbi wa Bunge kwa ajili ya kikao cha bunge hilo, mjini Dodoma leo.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri wa Fedha, Saada Salum Mkuya, akila kiapo mbele ya Mwenyekiti wa bunge hilo, Samuel Sitta (kushoto) kwa ajili ya kulitumikia kwa uaminifu na utiifu. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, akiwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kwenye ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma leo. 

Baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho (kushoto) na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (kulia) wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, alipokuwa akiwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba.
Baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri wa Sheria na Katiba, Asha Rose Migiri (kushoto) na wa Zanzibar, Abubakar Khamis Bakar (kulia) wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, alipokuwa akiwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba.
Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, akiwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kwenye ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma leo. 
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (kulia), akimweleza jambo mjumbe mwenzake, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenista Muhagama, ukumbini humo.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho (kushoto), Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (kulia) na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Jenista Muhagama, wakifurahia jambo, wakati Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, alipokuwa akiwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba.
Ukumbi wa Bunge, ulivyokuwa ukionekana wakati Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, alipokuwa akiwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba ndani ya ukumbi huo kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, mjini Dodoma. 
Ukumbi wa Bunge, ulivyokuwa ukionekana wakati Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, alipokuwa akiwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba ndani ya ukumbi huo kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, mjini Dodoma. 
Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, akiwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kwenye ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma leo. 
Baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, wakipiga makofi na mayowe na wengine kusimama wima, wakati Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, alipokuwa akiwasilisha na kufafanua baadhi ya vifungu vya Rasimu ya Pili ya Katiba.
Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, akiwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kwenye ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma leo. 
Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, akiwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kwenye ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma leo. 
Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, akiwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kwenye ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma leo. 

Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mkuu mstaafu Augustino Ramadhan, akizungumza na wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, wakati Mwenyekiti wake, alipofika ukumini humo kuwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba leo.

NA Zamaradi Kawawa, Maelezo Dodoma
Mwenyekiti aw Tume ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba ameliambia bunge Maalum la Katiba linaloendelea mkoani Dodoma kuwa Rasimu ya Katiba mpya inapendekeza Mawaziri wasitokane na wabunge.

Amesema hatua hii inamuondoa Rais kwenye bunge kwani kwa kuwa na Mawaziri ndani ya bunge Hilo kunalifanya bunge kushindwa kuisimamia serikali ipasavyo kwa kuwa serikali ni sehemu ya bunge Hilo.

Amesema Mawaziri watateuliwa na na Rais NA kuthibitishwa na bunge . Aidha , rasimu ya Katiba inapendekeza kuwa Rais achaguliwe kwa kupata kura zaidi ya asilimia 50 ya kura zote .

Rais Mara baada ya uchaguzi na kutangazwa na Tume ya uchaguzi anaweza kufikishwa mahakama ya rufaa kuhoji uhalali wake na mgombea yeyote wa kiti hicho aliyeshindwa na Shauri hilo kuamuliwa ndani ya mwezi mmoja.

Jaji Warioba amesema Rasimu ya Katiba inapendekeza kuwepo NA ukomo wa wabunge wa miaka 15 ya kukalia kiti hicho mfululizo ili kuondoa dhana ya umiliki wa ubunge na kuimarisha uwajibikaji.

Hakutakuwepo na uchaguzi mdogo endapo Mbunge atafariki badala yake nafasi hiyo itazibwa na jina litakalokuwa kwenye orodha zilizoandaliwa NA vyama vya siasa vyenye wabunge husika na kuwasilishwa kwa Tume ya Uchaguzi.

Aidha, Spika na Naibu Spika hawatatokana na Mawaziri, Naibu Waziri na wabunge ili kupata viongozi ambao hawataelemea upande wowote.

No comments:

Post a Comment