* Ikiendelezwa vizuri ni chanzo kikubwa cha ajira kwa vijana
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu, Bi. Joyce Fisoo akionyesha moja ya picha zinazotolewa na wadau wa filamu kama matangazo ya kutambulisha filamu zao sokoni. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Bi. Consilia Niyibitanga.
Na Georgina Misama-MAELEZO
SERIKALI imesema inatambua Tasnia ya Filamu
ikiendelezwa vizuri ni chanzo kikubwa cha ajira kwa vijana na ni njia madhubuti
ya kukuza uchumi kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa kitenngo cha mawasilianao
serikalini Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Concilia Niyibitanga
wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyikia ukumbi wa Idara ya habari
MAELEZO.
Concilia alisema kuwa mwamko unaongezeka kwa wasanii
na watengenezaji wa filamu kutoka ndani na nje ya nchi.
Hii inajidhihirisha kwa idadi ya vibali vya
utengenezaji filamu imeongezeka kutoka 100 mwaka 2000 hadi 472 Januari 2014.
Aidha, kampuni
zinazojishughulisha na uendeshaji wa shughuli za filamu nchini zimeongezeka
kutoka Kampuni moja ya Filamu Tanzania (TFC) na kufikia 129 mwaka 2013.
Kwa upande wa watengenezaji wa filamu za ndani,
uwasilishaji wa ukaguzi umeongezeka kutoka filamu 96 mwaka 2000 hadi kufikia
1059 Februari 2014.
Naye Katibu Mtendaji wa Bodi ya filamu nchini Joyce Fisoo
alitoa rai kwa wasanii wa filamu kutumia lugha ya Kiswahili hasa katika
uandaaji wa jina ili kulinda na kuikuza lugha yetu ya Kiswahi.
Tasnia ya Filamu nchini ilianza tangu mwaka 1920
wakati wa ukoloni, baada ya Uhuru, Serikali ya Tanzania kupitia bunge iliamua
kutunga sheria namba 4 ya mwaka 1976 ya Filamu na Michezo ya kuigiza ili kuweka
usimamizi mzuri wa tasnia hiyo.
No comments:
Post a Comment