Wachimba madini sita karibu na mji wa Johannesburg nchini Afrika kusini wanaoelezwa kuwa haramu wametoka katika shimo la mgodi walimokuwa wamenasa, kukiwa na hofu kuwa wengine zaidi wamenasa ndani ya shimo hilo.
Wachimbaji hao wameelezwa kutoka baada ya kile kilichoelezwa kupungua kwa vitisho vya kukamatwa mara watakapotoka shimoni, vitisho ambavyo awali viliwafanya wengine walionasa kukataa kutoka.
Shughuli rasmi za uokoaji zilisitishwa siku ya jumapili baada ya wachimbaji 11 kukubali kutoka.Mmoja wa wachimbaji alisikika akiwajulisha wenzake kuwa nje ya shimo hilo ni salama kwa kuwa askari hawapo katika eneo hilo.
wachimbaji wengine waligoma kutoka kutokana na tishio la kukamatwa na polisi.
Wachimbaji 11 waliokubali kutoka hivi sasa wanakabiliwa na mashtaka ya kuendesha shughuli za uchimbaji madini kinyume cha sheria.
No comments:
Post a Comment