Taarifa kutoka Sudan Kusini zinaelezea kuwepo mapigano ambayo yanakiuka mkataba uliosainiwa awali kati ya pande mbili hasimu kwenye mgogoro huo kusitisha vita.
Lakini huku pande hizo zikilaumiana raia wa kawaida wameathirika huku mji wa Bor ukishuhudia mauaji mabaya zaidi.Serikali inayoongozwa na Rais Salva Kiir imeendelea kulaumiana na waasi wanaoongozwa na aliyekuwa makamu wa rais Riak Machar.
Awali serikali ilitangaza kuanza kuzika miili iliyotapakaa katika barabara za mji huo.
Shughuli ya kuokota na kukusanya na kuizika miili iliotoapakaa mjini Bor imeanza. BBC imetembelea eneo kutakofanyika maziko ya pamoja nje kidogo ya mji huo.
Ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa pande zote mbili kwenye mgogoro wa Sudan Kusini, zimetenda uhalifu ikiwemo mauaji ya halaiki.
Tayari mamia ya watu wamezikwa katika kaburi la pamoja huku miili mingine ikisubiri kuzikwa.
Meya wa mji wa Bor Nhial Majak Nhial, anasema kuwa kaburi la tatu tayari limejaa miili na kaburi lengine litachimbwa likihitajika.
Yeye ndiye aliyeongoza juhudi za kukokota miili kutoka kando ya barabara za mji huo , vichakani na hata kutoka majumbani ili kuizika katika kaburi la pamoja.
Hadi kufikia sasa wameweza kuokota miili 500. Kwa mujibu wa Meya, nyingi ya miili imeanza kuoza kwani baadhi iliteketea.
Meya alisema kuwa wengi wa watu waliozikwa katika makaburi hayo walikuwa wakazi wa mji huo ambao wanajeshi na waasi walipigania kila upande ikiuteka mara tatu tangu ghasia kuzuka nchini humo Disemba mwaka jana.
Serikali sasa inaudhibiti mji huo.
No comments:
Post a Comment