Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema anaunga mkono amiri mkuu wa majeshi ya Misri Abdul Fattah al-Sisi Kuwania urais wa taifa hilo.
Putin alimweleza Al-Sisi kuwa alifahamu kuhusiana na niya yake ya kuwania urais.
Kiongozi huyo wa jeshi la Misri ndiye aliyeongoza mapinduzi yaliyomng'oa mamlakani aliyekuwa rais wa Misri Mohammed Morsi mwezi julai mwaka uliopita.Hata hivyo hakujakuwa na dhibitisho lolote kutoka kwa ujumbe wa serikali ya Misri.
Katiba mpya ya taifa hilo inashurutisha kufanyika kwa uchaguzi ifikiapo katikati ya mwezi Aprili mwaka huu.
Kheri Njema
Mwandishi wa BBC anasema iwapo uchaguzi wa urais utafanyika sasa kiongozi huyo wa jeshi anapigiwa upatu kushinda kwa sababu ya umaarufu wake .
Aidha hakujajitokeza mpinzani mwenye ushawishi mkubwa .
Putin
""nakutakia kheri na ufanisi katika juhudi zako kwa niaba yangu binafsi na wananchi wa Urusi ''"
Field Marshal Sisi yuko mjini Moscow kujadili mkataba wa silaha wenye thamani ya dola bilioni 2 .
Mkataba huo unawadia baada ya serikali ya Marekani kusitisha makubaliano ya Mauzo ya silaha na Misri baada ya kungolewa madarakani kwa aliyekuwa rais Mohammed Morsi mwezi julai mwaka uliopita.
No comments:
Post a Comment