Polisi wenye silaha mjini Iringa, wakijiandaa kuzuia msafara wa mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga Iringa, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bi. Grace Mvanga jana kwa madai ya kufanya maandamano yasiyo na kibali.
Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga kupitia Chadema, Bi. Grace Mvanga akipita eneo la kuzuizi cha Polisi baada ya kuruhusiwa kupita eneo hilo la mlima Ipogolo, mjini Iringa jana.
Polisi Iringa wakiwa wameuzuia msafara wa mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga, Bi Grace Mvanga jana kwa madai ya kufanya maandamano bila ya kibali cha Polisi. Mgombea huyu alizuiliwa kwa muda wa dakika kama 20 kabla ya kuruhusiwa kupita na wafuasi wake.
Diwani wa Kata ya Mvinjeni, Iringa mjini, Bw. Frank Nyalusi (Chadema), kati akiwa chini ya ulinzi wa Polisi jana baada ya Polisi kuzuia msafara wa mgombea wa Chadema Jimbo la Kalenga Bi. Grace Mvanga eneo la mlima wa Samora, mlima wa Ipogolo mjini Iringa (Picha zote kwa hisani ya Blog ya Francis Godwin)
No comments:
Post a Comment