TANGAZO


Tuesday, February 18, 2014

Nigeria:Jeshi lasema liko ngangari



Wanajeshi wa Nigeria vitani na Boko Haram
Jeshi la Nigeria limesema kuwa litaendelea na harakati zake dhidi ya kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Boko Haram licha ya kundi hilo kufanya mashambulizi mabaya dhidi ya raia wasio na hatia siku ya Jumatatu katika jimbo la Borno.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika jimbo la Borno, wapiganaji hao waliwaua watu 105 akiwemo nyanya mmoja aliyekuwa anajaribu kumlinda mjukuu wake kutokana na mashambulizi.
Jeshi linasema kuwa magaidi hao ambao hulenga kijiji baada kingine na kufanya mashambulizi ya kuvizia, ni wale wanaotoroka mashambulizi ya majeshi katika maficho yao mpakani mwa nchi hiyo na nchi jirani.Boko Haram pia waliwaua wanajeshi 9 wiki jana.
Majeshi yanasemekana kuongeza kasi ya mashambulizi ya angani na ardhini dhidi ya Boko Haram katika maficho yao ya misituni na maeneo yaliyoathirika na sehemu zingine za nchi Kaskazini Mashariki ambako Boko Haram wanajificha.
Jeshi limesema katika taarifa yao kuwa Majeshi ya usalama yataendelea kutumia nguvu kadri ya uwezo wao kuhakikisha kuwa operesheni yao dhidi ya magaidi hao inafanikiwa.
Wakati huohuo wanajeshi wanadhibiti ilinzi wa maeneo ambayo yanakabiliwa na tisho la mashambulizi pamoja na kutumia vifaa vya elektroniki kudhibiti usalama.
Wanajeshi wamefanikiwa kuwakamata baadhi ya washukiwa wa mauaji ya hivi karibuni na kupokonywa silaha huku wakisubiri hukumu.

No comments:

Post a Comment