TANGAZO


Tuesday, February 18, 2014

MARADONA AWAFUNDA MAN UNITED DUBAI

WACHEZAJI wa Manchester United wamekutana na kuzungumza naye, gwji wa soka duniani, Diego Maradona katika kambi yao ya mazoezi nchini Dubai.

Kiungo huyo mstaafu wa Argentina, maarufu zaidi kwa 'Mkono wa Mungu' kutokana na kuifunga bao la mkono England katika Fainali za Kombe la Dunia mwaka 1986, alikutana na nyota hao walioweka kambi ya wiki moja huko.

Robin van Persie, Juan Mata, Rio Ferdinand na David de Gea walikuwa miongoni mwa wachezaji wa United waliopiga picha na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 53, ambazo waliziposti kwenye mitandao yao ya kijamii. 
Babu kubwa: Kiungo wa Hispania, Juan Mata hakukosa nafasi ya kupicha picha na Maradona
Hitmen: Dutch striker Robin van Persie described Diego Maradona as his 'hero'
Mkali wa mabao: Mshambuliaji wa Uholanzi, Robin van Persie akiwa na Diego Maradona ambaye ni shujaa wake

Maradona ni kipenzi cha wengi miongoni mwa wapenzi na wadau wa soka, wakiwemo wachezaji wenyewe na Mata na Van Persie wamesema wao ni mashabiki wa wakubwa wa gwiji huyo.
Nyota hao wawili wa United walishindwa kuficha furaha yao baada ya kumuona Maradona akiwasili kwenye viwanja walivyokuwa wanafanya mazoezi na haraka wakaenda kuposti juu ya mchezaji huyo wa zamani wa Boca Juniors kwenye Twitter.
"Mabibi na mabwana, mtumia mguu wa kushoto bora daima! EL DIEGO. #Maradona," alisema Mata.
Van Persie alisema: "Babu kubwa kukutana na shujaa wangu tena, Diego bora daima,". 
Maradona alikuwa hatari sana anapoingia kwenye eneo la mita 18 la wapinzani na haikuwa ajabu Ferdinand na de Gea walitumia fursa hiyo kupata ushauri kutoka kwa mkali huyo wa zamani wa Argentina.Helping hand: Diego Maradona popped down to Man United's warm weather training session in Dubai
Diego Maradona akiwa na Ferdinand Dubai
Hands of God? United keeper David de Gea poses for his picture with Argentina legend Maradona
Kipa wa United, David de Gea akiwa na Maradona

Ferdinand aliposti picha akiwa na Maradona kwenye Instagram yake, akiambatanisha na maelezo: "Mimi na #Gwiji#DiegoMaradona #Mkuu".
Kipa De Gea ameandika: "Babu kubwa kuwa namba 10 bora!! "El Pelusa"'
Nyota huyo wa Amerika Kusini yupo kwa muda mrefu Dubai na amekuwa kocha wa Al Wasl FC inayoshiriki ya Ligi ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), hadi mwaka 2012.
United imefuata hali ya hewa ya joto Dubai ili kufanya mazoezi ya wiki moja.

No comments:

Post a Comment